Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 IKAWA huko Ikonio wakaingia pamoja katika sunagogi ia Wayahudi, wakanena; hatta jamaa kubwa ya Wayahudi na ya Wayunani wakaamini.

2 Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.

3 Bassi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa uthabiti katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao.

4 Lakini jamii ya watu wa mjini wakagawanyikana: bawa walikuwa upande wa Wayahudi, na hawa upande wa Mitume.

5 Hatta palipotokea shambulio la watu wa mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga mawe,

6 bassi, wakapata khabari wakakimbilia miji ya Lukaonia. Lustra na Derbe, na inchi zilizo kando kando:

7 wakakaa huko, wakiikhubiri Injili.

8 Na huko Lustra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mama yake, ambae hajaenda kabisa.

9 Mtu huyo alimsikia Paolo akinena; nae akamkazia macho akaona ya kuwa ana imani ya kuponywa,

10 akanena kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawa sawa. Akasimama upesi akaenda.

11 Na makutano walipoona aliyoyafanya Paolo wakapaaza sauti zao, wakisema kwa Kilukaonia, Mungu wametushukia kwa mifano ya wana Adamu.

12 Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paolo, Herme, kwa sababu ndiye aliyetakadamu katika kimena.

13 Kuhani wa Zeu ambae hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ngʼombe na taji za maua hatta malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano.

14 Walakini mitume Barnaba na Paolo, walipopata khabari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakipiga kelele, wakisema, Akina hwana, mbona mnafanya haya?

15 Sisi nasi tu wana Adamu hali moja na ninyi; twawakhubiri khabari njema mgenke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hayi, aliyeumba mbingu na inchi na bahari na vitu vyotc vilivyomo:

16 ambae zamani zilizopita aliwaacha mataifa yote waende katika njia zao wenyewe.

17 Illakini hakujiacha hana shahidi kwa kuwa alitenda mema akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwajaza mioyo yenu chakula na furaha.

18 Na kwa maneno haya wakawazuia makutano kwa shidda, wasiwatolee dhabihu.

19 Wayahudi wakalika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hatta wakampiga mawe Paolo wakamhurura nje ya mji, wakidhani ya kuwa amekwisha kufa.

20 Lakini wanafunzi walipokuwa wakimzunguka pande zote, akasimama, akaingia ndani ya mji; na siku ya pili yake akatoka, akaenda zake pamoja na Barnaba hatta Derbe.

21 Hatta walipokwisha kuikhubiri Injili katika niji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea hatta Lustra na Ikonio na Antiokia,

22 wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.

23 Na walipokwisha kuchagua wazee katika killa mji, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka kafika mikono ya Bwana waliyemwamini.

24 Wakapita kati ya Pisidia wakamgia Pamfulia.

25 Na baada ya kukhubiri katika Perga wakatelemka hatta Attalia.

26 Na kutoka huko wakasafiri baharini kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.

27 Hatta walipolika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwaruba amewafungulia mataifa mlango wa imani.

28 Wakashinda huko wakati usio mchache, pamoja na wanafunzi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo