Matendo 12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 PANAPO majira yaleytile Herode mfalme tw akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa Kanisa. 2 Akamwua Yakobo ndugu wa Yohana kwa upauga. 3 Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamtwaa na Petro. Siku hizo ndizo siku za mikate isiyochachwa. 4 Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa askari wanewane, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa mbele ya watu. 5 Bassi Petro akalindwa gerezani, sala zikawa zinafanyika kwa juhudi sana na Kanisa mbele za Mungu kwa ajili yake. 6 Hatta wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku uleule. Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili: walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. 7 Marra malaika wa Bwana akasimama karibu nae, nuru ikamulika chumbani mle, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo ikamwanguka. 8 Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu: akafanya hivyo. Akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. 9 Akatoka, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni khabari ya kweli iliyofanyika na malaika; bali alidhani anaona njozi. 10 Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hatta mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia. Wakatoka, wakapita katika njia moja; marra malaika akamwacha. 11 Hatta Petro alipofahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na kutazamia kwa taifa la Wayahudi. 12 Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mama yake Yohana, ambae jina lake la pili ni Marko; na wafu wengi wamekutana wakiomba. 13 Na Petro alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Rhoda, akaja kusikiliza. 14 Alipoitambua sauti ya Petro, hakulifungua lango kwa furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango. 15 Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo bivyo. 16 Wakanena, Ni malaika wake. Petro akafuliza kugonga; hatta walipokwislia kumfungulia wakamwona, wakastaajabu. 17 Nae akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Enendeni, mkampashe Yakobo na ndugu zetu khabari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine. 18 Hatta kulipopambazuka askari wakaingiwa na fadhaa nyingi, amekuwaje Petro. 19 Na Herode alipomtafuta, asimwone, akawauliza walinzi, akaamuru wanawe. Nae akatelemka kutoka Yahudi kwenda Kaisaria, akakaa huko. 20 Nae Herode aliwakasirikia sana watu wa Tʼuro na Sidon: wakamwendea kwa nia moja, na wakiislia kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulalia, wakataka amani; kwa maana inchi yao ilipata riziki kwa inchi ya mfalme. 21 Bassi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifaume, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa khotuba. 22 Watu wakapiga kelele, wakinena, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwana Adamu. 23 Marra malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu: akaliwa na funza, akatoa roho. 24 Neno la Bwana likazidi na kuenea. 25 Na Barnaba na Saul, walipokwisha kuitimiza khuduma yao, wakarejea kutoka Yerusalemi wakamchukua pamoja nao Yohana aitwae Marko. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania