Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI mitume na ndugu waliokuwa katika Yahudi wakapata khabari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Bwana.

2 Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemi, wale walio wa Tohara wakashindana nae, wakisema,

3 Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao.

4 Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema,

5 Nalikuwa katika mji wa Yoppa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kama nguo kubwa kikishuka, kinashushwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.

6 Nikaitazama sana, nikifikiri, nikaona nyama za inchi zenye miguu mine, Ua nyama za mwituni, nazo zitambaazo, na ndege za anga.

7 Nikasikia sauti ikiniambia, Ondoka, Petro, ukachinje ule.

8 Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najis hakijaingia kinywani mwangu.

9 Sauti ikanijibu marra ya pili kutoka mbinguni, Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najis.

10 Jambo hili likatendeka marra tatu, kiisha vitu vyote vikavutwa juu tena mbinguni.

11 Kumbe! marra hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba niliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria.

12 Roho akaniambia nifuatane nao, nisione mashaka. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule:

13 akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yoppa ukamwite Simon, aitwae Petro

14 atakaekuambia maneno ambayo utaokolewa nayo, wewe na nyumba yako yote.

15 Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.

16 Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.

17 Bassi ikiwa Mwenyiezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?

18 Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.

19 Bassi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile shidda iliyotukia kwa khabari ya Stefano, wakasafiri hatta Foiniki na Kupro na Antiokia, wasilikhubiri lile neno illa kwa Wayahudi peke yao.

20 Baadhi ya hao walikuwa watu wa Kupro na Kurene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wahelenisti, wakakhubiri khabari njema za Bwana Yesu.

21 Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao: watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana.

22 Khabari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wakaintuma Barnaba, aende hatta Antiokia.

23 Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.

24 Maana alikuwa mtu mwema, amejaa Roho Mtakatifu na imani: watu wengi wakajitia upande wa Bwana.

25 Barnabi tikatoka akaenda Tarso kumtafuta Saul: hatta alipokwisha kumwona akamleta Antiokia.

26 Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hajio Antiokia.

27 Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yemsalemi hatta Antiokia.

28 Akasimama mmojawapo wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa nweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima; nayo ikatukia katika siku za Klaudio Kaisari.

29 Na wale wanafunzi, killa mtu kwa kadiri alivyofanikiwa wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Yahudi.

30 Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaha na Saul.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo