Marko 9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 AKAWAAMBIA, Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa ambao hawataonja mauti hatta watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu. 2 Hatta baada ya siku sita Yesu akawachukua Petro, na Yakobo, na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu kwa faragha peke yao: 3 akageuka sura yake mbele yao: mavazi yake yakawa yakimetameta, meupe kwa mfano wa thuluji, jinsi asivyoweza fundi duniani kuyafanya meupe. 4 Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakisemezana na Yesu. 5 Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabbi, ni vizuri sisi kuwapo hapa: na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja eha Eliya. 6 Maana yake hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na khofu nyingi. 7 Likawako wingu, likawatia uvuli: sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ui Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. 8 Na marra hiyo walipotazama huku na huku, hawakumwona mtu, illa Yesu peke yake pamoja nao. 9 Walipokuwa wakishuka mlimani akawaagiza wasimweleze mtu waliyoyaona, illa Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu. 10 Wakalishika neno lile, wakiulizana wao kwa wao, Huku kufufuka katika wafu maana yake nini? 11 Wakamhoji, wakinena, Waandishi wanena ya kuwa imempasa Eliya kuja kwanza. 12 Akajihu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kutengeneza yote; lakini, pamoja na haya ameandikwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharanliwa? 13 Lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa. 14 Hatta alipowafikia wanafunzi wake, akaona makutano mengi wakiwazunguka na waandishi wakijadiliana nao; 15 marra makutano yote wakimwona wakashangaa wakamwendea mbio, wakamsalimu. 16 Akawauliza wale waandishi, Nini mnajadiliana nao? 17 Mtu mmoja katika makutano akamjibu, Nalimieta mwana wangu kwako, ana pepo bubu: 18 na killa ampagaapo, humrarua: nikasema na wanafunzi wako wapate kumfukuza, wasiweze. 19 Akamjibu, akanena, Ee kizazi kisichoamini, niwe kwenu hatta lini? nichukuliane nanyi hatta lini? Mleteni kwangu. 20 Wakanileta kwake: hatta alipomwona marra yule pepo akamrarua: akaanguka chini, akagaagaa, akitoka povu. 21 Akamwuliza baba yake, Tangu wakati gani amepatwa na haya? Akasema, Tangu utoto. 22 Na marra nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno, utuhurumie, utusaidie. 23 Yesu akamwambia, Ukiweza kuamini: yote yawezekana kwake aaminiye. 24 Marra baba yake yule kijana akapaaza sauti, machozi yakimtoka, akanena, Naamini, Bwana, nisaidie kutokuamini kwangu. 25 Nae Yesu akiona ya kuwa makutano yanakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu ua kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke, wala usimwingie tena. 26 Akalia, akamrarua sana, akamtoka: akawa kama amekufa: hatta wengi wakasema, Amekufa. 27 Lakini Yesu akamshika mkouo akamwinua; nae akasimama. 28 Hatta alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumfukuza? 29 Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kusali na kufunga. 30 Wakatoka huko, wakapita kati kati ya Galilaya: nae hakutaka mtu ajue. 31 Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akiwaambia ya kwamba Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hatta akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka. 32 Nao hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza. 33 Wakafika Kapernaum: hatta alipokuwa nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani? 34 Wakanyamaza. Kwa maana walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa. 35 Akaketi chini akawaita wathenashara akawaambia, Mtu atakae kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mkhudumu wa wote. 36 Akatwaa kitoto, akamweka kati kati yao, akamkumbatia, akawaambia, 37 Mtu akimpokea kitoto kimoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, hanipokei mimi, bali yeye aliyenituma. 38 Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akifukuza pepo kwa jina lako, nae hatufuati sisi: tukamkataza, kwa sababu hatufuati sisi. 39 Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakaefanya mwujiza kwa jina langu akaweza wakati huo huo kuninena mabaya; 40 kwa sababu asiye kiuyume chetu, ni upande wetu. 41 Kwa kuwa ye yote atakaewanywesha ninyi kikombe cha maji kwa jina langu, kwa kuwa ninyi watu wa Kristo, amin nawaambieni hatakosa thawabu yake. 42 Na ye yote atakaemkosesha mmoja katika wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. 43 Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni kheri kuiingia katika uzima u kilema, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehannum, kwenye moto usiozimika; 44 ambao funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate: ni kheri kuingia katika uzima, umepungukiwa mguu, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jebannum, katika moto usiozimika; 46 ambao funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 47 Na jicho lako likikukosesha, litupe: ni kheri kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehannum ya moto: 48 ambapo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 49 Kwa sababu killa mtu atatiwa chumvi kwa moto, na killa dhabihu itatiwa chumvi kwa chumvi. 50 Chumvi ni njema; lakini chumvi ikitokwa na ladhdha yake, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania