Marko 8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 TENA siku zile, kwa kuwa mengi mno makutano, nao hawana kitu cha kula, Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, 2 Nawahurumia makutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula: 3 hatta nikiwaaga waende zao nyumbani kwao wanafunga, watazimia njiani: na baadhi yao wametoka mbali. 4 Wanafunzi wake wakamjibu, Atawezaje mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani? 5 Akawauliza, Mikate mingapi mnayo? Wakasenia, Saba. 6 Akawaagiza makutano waketi chini: akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandalie: wakawaandalia makutano, 7 Walikuwa na visamaki vichache; akavibariki, akasema, na hivi waviandae. 8 Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba. 9 Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga. 10 Marra akapanda chomboni pamoja na wanafunzi wake, akaenda pande za Dalmanutha. 11 Wakatokea Mafarisayo wakaanza kuhujiana nae; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu. 12 Akaugua rohoni mwake, akanena, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki. 13 Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hatta ngʼambu. 14 Wakasahan kuchukua mikate, wala chomboni hawana illa mkate mmoja tu. 15 Akawaagiza, akisema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode. 16 Wakabishana wao kwa wao, kwa kuwa hawana mikate. 17 Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana kwa sababu hamna mikate? Hamfahamu bado, wala hamjaelewa? Mioyo yenu i migumu hatta sasa? 18 Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? wala hamkumbuki? 19 Nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Thenashara. 20 Na ile saba kuwapa wale elfu nne, mlichukua makanda mangapi yamejaa vipande? Wakamwambia, Saba. 21 Akawaambia, Imekuwaje hamjafahamu? 22 Wakalika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. 23 Akamshika mkono vule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akaweka mikono yake juu yake, akamwuliza, Waona kitu? 24 Akatazama juu, akanena, Naona watu kama miti, inakwenda. 25 Ndipo akaweka mkono wake juu yake marra ya pili machoni mwake, akamwagiza atazame juu; akapata kuwa mzima, akaona wote waziwazi, wajapokuwa mbali. 26 Akampeleka nyumbani kwake, akinena, Usiingie mjini, wala usiseme na mtu mjini. 27 Akatoka Yesu na wanafunzi wake wakaenda vijiji vya Kaisaria ya Filipo: hatta njiani akawauliza wanafunzi wake, akiwaambia, Watu huninena mimi ni nani? 28 Wakamjibu, Yohana Mbatizaji; wengine Eliya; wengine mmojawapo wa manabii. 29 Yeye akawauliza, Na ninyi mnasema ya kuwa mimi ni nani? Petro akamjibu akamwambia, Wewe ndiwe Kristo. 30 Akawaagiza wasimwambie mtu khabari zake. 31 Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na makuhani, wakuu na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka. 32 Petro akamchukua akaanza kumkemea. 33 Akageuka akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akinena, Enenda zako nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, hali ya wana Adamu. 34 Akawaita makutano na wanafunzi wake, akawaambia, Atakae kuniandama na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate. 35 Kwa maana atakae kuisalimisha roho yake, ataiangamiza, na mtu atakaeitoa roho yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili, huyu ataisalimisha. 36 Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote akapata khasara ya roho yake? 37 Ama mtu atoe nini badala ya roho yake? 38 Maana killa mtu atakaenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha zina na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya yeye atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania