Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KIISHA Mafarisayo na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemi wakakusanyika mbele yake,

2 wakaona baadhi ya wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najis, yaani, yasiyonawiwa, wakawalaumu.

3 Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono kwanza, hawali, wakishika hadithi za wazee wao:

4 tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyushika kama vile kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba na meza.

5 Bassi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuzifuata hadithi za wazee, bali hula chakula kwa mikono najis?

6 Akawaambia, Isaya aliwakhubiri vema ninyi wanaliki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa hunibeshimu kwa midomo, Bali mioyo yao iko mbali nami;

7 Lakini waniabudu ibada ya burre, Wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wana Adamu.

8 Kwa maana mmeiacha amri ya Mungu, na kuzishika hadithi za wana Adamu, kuosha midumu na vikombe: na mengine mengi ya namna hii mwayafanya.

9 Akawaambia, Mwaikataa vema amri ya Mungu mpate kushika hadithi zenu.

10 Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanae baba yake au mama yake na afe.

11 Bali ninyi hunena, Mtu akimwambia baba yake au mama yake, Ni Korban (yaani kimewekwa wakfu) kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho:

12 wala hamrukhusu baada ya hayo kumtendea neno baba yake wala mama yake;

13 mkilitangua neno la Mungu kwa hadithi yenu mliyohadithia; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.

14 Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote, fahamuni.

15 Hapana kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia najis, bali vimtokayo, ndivyo vimtiavyo najis yule mtu.

16 Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.

17 Hatta alipoingia nyumbani, amewaacha makutano, wanafunzi wake wakamwuliza khabari za ule mfano.

18 Akawaambia, Hivi na ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kuwa killa kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia najis;

19 kwa sababu hakimwingii moyoni, illa tumboni tu; kiisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.

20 Akanena, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho najis.

21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, zina, asharati,

22 wizi, uuaji, tamaa mbaya, hila, jeuri, kijicho, matukano, kiburi, upumbafu.

23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu najis.

24 Akaondoka huko, akaenda zake hatta mipaka ya Turo na Sidon. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kustirika.

25 Kwa sababu mwanamke, ambae binti yake yuna pepo mchafu, alisikia khabari zake, akaja akamwangukia miguu.

26 (Na vule mwanamke ni Myunani, kabila yake Msurofenissa). Akamwomba amfukuze pepo katika binti yake.

27 Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza: maana si vema kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa.

28 Nae akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hatta mbwa chini ya meza hula makombo ya watoto.

29 Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, nenda zako; pepo amemtoka binti yako.

30 Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka.

31 Akatoka tena katika mipaka ya Turo akapita katikati ya Sidon, akaenda hatta bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli.

32 Wakamletea kiziwi, nae ana kigugumizi, wakamsihi aweke mikono yake juu yake.

33 Akamtenga na makutano kwa faragha, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa nlimi,

34 akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Effatha, maana yake, Funguka!

35 Marra masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.

36 Akawaagiza wasimwambie mtu; lakini kwa kadiri alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza khabari, wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena,

37 Ametenda yote vizuri; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo