Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKATOKA huko, akafika hatta inchi ya kwao: wanafunzi wake wakamfuata.

2 Ilipokuwa sabato, akaanza kufundisha katika sunagogi: wengi wakisikia, wakashangaa, akinena, Huyu amepata wapi haya? Na, Hekima gani hii aliyopewa huyu, na nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?

3 Huyu si yule sermala, mwana wa Mariamu, na ndugu wii Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simon? na ndugu zake wanawake hawapo hapa petu? Wakachukizwa nae.

4 Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, illa katika inchi yake, na kwa jamaa zake, na katika nyumba yake.

5 Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya.

6 Akastaajahu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.

7 Akawaita wale thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili; akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu:

8 akawaagiza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa gongo tu, wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni:

9 lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili.

10 Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hatta mtakapotoka mahali pale.

11 Na watu wote wasiokaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakungʼuteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu kuwa ushuhuda kwao.

12 Wakatoka, wakakhubiri kwamba watu watubu.

13 Wakafukuza pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagoujwa, wakawaponya.

14 Mfalme Herode akasikia khabari; kwa maana jina lake limepata kutangaa, akanena, Yohana Mbatizaji amefufuka, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake. Wengine walinena, Yu Eliya.

15 Wengine walinena, Huyu ni nabii au kama mmoja wa manabii.

16 Lakini Herode aliposikia, alinena, Huyu ndiye Yohana, niliyemkata kichwa; amefufuka.

17 Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma wata, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili va Herodias, nikewe Filipo ndugu yake: kwa kuwa amemwoa; bassi Yohana alimwambia Herode,

18 Si halali kwako kuwa na mke wa ndugu yako.

19 Bassi yule Herodias akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate.

20 Maana Herode alimwogopa Yohana: hatta akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamhami, na alipokwisha kumsikiliza alifanya mambo mengi: nae alikuwa akimsikiliza kwa furaha.

21 Hatta ilipotokea siku ya kufaa, na Herode (siku kuu ya kuzaliwa kwake) alipowafanyia karamu masheki na majemadari na watu wakubwa wa Galilaya,

22 ndipo binti yake yule Herodias akaingia, akacheza, akampendeza Herode nao walioketi pamoja nae karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lo lote utakalo, nitakupa.

23 Akamwambia, Lo lote utakaloniomba, nitakupa hatta nussu ya ufalme wangu.

24 Akatoka, akamwambia mama yake, Niombe nini? Akasema, Kichwa cha Yohana Mbatizaji.

25 Marra akaingia kwa haraka mbele ya mfalme akaomba akinena, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.

26 Mfalme akafanya huzuni sana, lakini kwa ajili ya nyapo zake, na kwa ajili yao walioketi karamuni, hakutaka kumkataa.

27 Marra mfalme akatuma askari, akiamuru kuleta kichwa chake.

28 Akaenenda, akamkata kichwa mle gerezani, akaleta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, yule kijana akampa mama yake.

29 Wauafunzi wake waliposikia khabari, wakaenda, wakachukua mayiti yake, wakamzika.

30 Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa khabari za mambo yote waliyoyafanya na mambo yote waliyoyafundisha.

31 Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipo watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hatta haikuwapo nafasi ya kula.

32 Wakaenda zao chomboni, mahali pasipo watu, kwa faragha.

33 Watu wakawaona wakienda zao, wengi wakamtambua, wakaenda huko mbio, toka miji yote, wakatanguha kufika, wakakusanyika mbele yake.

34 Yesu aliposhuka chomboni, akaona makutano mengi, akawahurumia, kwa sababu walikuwa kana kondoo wasio mchunga; akaanza kuwafundisha mengi.

35 Hatta zikapita saa nyingi za mchana, ikawa karibu na magharibi, wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Mahali hapa nyika tupu, na sasa kunakuchwa;

36 uwaage watu hawa, illi waende zao mashambani na vijijini huko na huko, wakajinunulie chakula.

37 Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula: Wakamwambia, Je! twende zetu tukanunue mikate ya dinari miateen tukawape kula?

38 Akawaambia, Mikale mingapi mnayo? Enendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakanena, Mitano, na samaki mbili.

39 Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabiehi.

40 Wakaketi kwa safu, nyingine mia, nyingine khamsimi.

41 Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama mbinguni, akavibariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake awaandikie: na zile samaki mbili akawagawia wote.

42 Wakala wote wakashiba.

43 Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu thenashara: navyo vipande vya samaki.

44 Na wanaume walioila ile mikate wapata elfu tano.

45 Marra akawashurutisha wanafunzi wake wapande chomboni, watangulie kwenda ngʼambu hatta Betsaida wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano.

46 Hatta alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kusali.

47 Ilipokuwa jioni chombo kilikuwa kati ya bahari, na yeye peke yake katika inchi kavu.

48 Akawaona wakitaahika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hatta yapata zamu ya nne ya usiku akawaendea akitemhea juu ya bahari; akataka kuwdpita.

49 Nao walipomwoua anatembea juu ya bahari walidhani ya kuwa ni kivuli, wakapiga yowe, kwa sababu wote walimwona, wakafadhaika.

50 Marra akasema nao, akawaambia, Jipeni moyo: ni mimi msiogope.

51 Akapanda mle cbomboni walimo; npepo ukakoma; wakashangaa sana, kupita kiasi, wakastaajabu;

52 kwa maana hawakufahamu khabari za ile mikate, walakini mioyo yao ilikuwa migumu.

53 Hatta walipokwisha kuvuka wakafika inchi ya Genesareti, wakatia nanga.

54 Na wakiisha kutoka chomboni, marra watu walimtambua, wakaenda mbio, wakizunguka inchi ile yote,

55 wakaanza kuwachukua walio hawawezi vitandani, kwenda killa mahali waliposikia kwamba yupo.

56 Na killa alikokwenda, akiingia vijijini, au mijini, au mashambani, wakawaweka wagonjwa sokoni, wakamsihi waguse walao upindo wa vazi lake: nao wote waliomgusa wakapona.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo