Marko 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 WAKAFIKA ngʼambu ya bahari hatta inchi ya Wageraseni. 2 Na alipokwisha kushuka chomboni, marra akakutwa na mtu ambae ametoka makaburini, nae ana pepo mchafu, makao yake yalikuwa pale makaburini: 3 wala hakuna mtu aliyeweza kumfunga, hatta kwa minyororo: 4 kwa sababu alikuwa amefungwa marra nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunjavunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Na siku zote, usiku na mchana, alikuwa makaburini na milimani, akilia na kujikata kwa mawe. 6 Alipomwona Yesu kwa mbali, akampiga mbio, akamsujudia; 7 akalia kwa sauti kuu akanena, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, uniapie kwa Mungu kwamba hutaniadhibu. 8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. 9 Akamwambia, Jina lako nani? Akajibu, akamwambia, Jina langu Legioni: kwa kuwa tu wengi. 10 Akamsihi sana asiwapeleke nje ya incbi ile. 11 Na pale milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, walisha. 12 Pepo wote wakamsihi, wakinena, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. 13 Akawapa rukhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale ngumwe: kundi lote likatelemka kwa kassi gengeni, wakaingia baharini; walikuwa wapata elfeen; wakafa baharini. 14 Wachungaji wa wale nguruwe wakakimbia wakaeneza khahari mjini na mashamba. Wakatoka waone khabari iliyotukia. 15 Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, nae ndiye aliyekuwa na ile legione; wakaogopa. 16 Nao walioona wakaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na khabari za nguruwe. 17 Wakaanza kumsihi atoke katika mipaka yao. 18 Alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi awe pamoja nae: 19 Yesu hakumrukhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawakhubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. 20 Akaenda zake, akaanza kukhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakataajabu. 21 Hatta Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ngʼambu katika kile chombo, wakamkusanyikia makutano mengi: nae alikuwa kando ya bahari. 22 Kumbe! akaja mtu mmoja katika wakuu wa sunagogi, jina lake Yairo: hatta alipomwona, akaanguka miguuni pake, 23 akimsihi sana, akinena. Binti yangu mdogo yu katika kufa: nakuomba nje, nweke mkono wako juu yake, apate kupona, nae ataishi. 24 Akaenda pamoja nae: makutano mengi wakamfuata, wakimsongasonga. 25 Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka thenashara, 26 na kuteswa mengi kwa mikono ya tabibu wengi, akagharimu vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hatta kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya, 27 bassi aliposikia khabari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; 28 maana alinena, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. 29 Marra chemchemi ya damu yake ikakauka, akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. 30 Marra Yesu akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya makutano, akanena, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? 31 Wanafunzi wake wakamwambia, Wawaona makutano wanavyokusongasonga, nawe wanena, Ni nani aliyenigusa? 32 Akatazama pande zote illi amwone yule aliyelitenda neno hili. 33 Na yule mwanamke akaingiwa na khofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. 34 Akamwambia, Binti imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, ukawe mzima, usiwe na msiba wako tena. 35 Hatta alipokuwa akisema wakaja watu kutoka kwa mkuu wa sunagogi, wakinena, Binti yako amekwisha kufa: ya nini kuzidi kumsumbua mwalimu? 36 Yesu, marra alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sunagogi, Usiogope, amini tu. 37 Wala hakumrukhusu mtu afuatane nae, illa Petro, na Yakobo, na Yohana ndugu yake Yakobo. 38 Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sunagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo mengi. 39 Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hakufa, bali amelala tu. Wakamcheka sana. 40 Nae alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa baba yake yule mtoto na mama yake, na wale walio pamoja nae, akaingia ndani alimokuwamo yule mtoto. 41 Akamshika mkono yule kijana, akamwambla, Talitha, kumi: tafsiri yake, Kijana, nakuambia, Ondoka. 42 Marra akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata miaka thenashara. Wakashangaa mshangao mwingi. 43 Akawaagiza sana, mtu asijue khabari ile; akaamuru apewe chakula. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania