Marko 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 AKAANZA kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkuliwa, hatta yeye akapanda chomboni, akakaa baharini; mkutano wote ulikuwako katika inchi kavu kando ya bahari. 2 Akawafundisha mengi kwa mifano, akawaambia katika mafundisho yake, 3 Sikilizeni: Mpanzi alitoka kwenda kupanda; 4 ikawa alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zikaangukia njiani, wakaja ndege wakazila. 5 Nyingine zikaanguka penye mwamba, pasipokuwa na udongo mwingi; marra zikamea kwa kuwa na udongo haba; 6 hatta jua lilipoznka zikaungua, na kwa kuwa hazina mizizi zikakauka. 7 Nyingine zikaanguka penye miiba: ile miiba ikakua, ikazisonga, zisizae matunda. 8 Nyingine zikaanguka panapo udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sittini, na moja mia. 9 Akanena, Aliye na masikio ya kusikilia, na asikie. 10 Alipokuwa peke yake, watu waliomzunguka, na wale thenashara wakamwuliza khabari za ule mfano. 11 Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu; hali wale walio nje yote huwawia kwa mifano, 12 illi wakitazama watazame, wasione; na wakisikia wasikie, wasifahamu; wasije wakageuka, wakasamehewa dbambi zao. 13 Askawaambia, Hamjui mfano huu? Bassi mifano yote mtaitambuaje? 14 Mpanzi yule hulipanda neno. 15 Hawa ndio walio njiani, lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, marra huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao. 16 Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye mwamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, marra hulipokea kwa furaha; 17 waki hawana mizizi ndani yao, hali hudumu muda mehache; kiisha ikitokea shidda au udhia kwa sababu ya lile neno, marra huchukizwa. 18 Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba, ni watu walisikiao lile neno, 19 na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai. 20 Na hawa ndio waliopandwa panapo udongo mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, moja thelathini, moja sittini, na moja mia. 21 Akawaambia, Mwaonaje? Taa huletwa illi kutiwa ehini ya kikapu, au ehini ya kitanda? si kutiwa juu ya kibao cha kuwekea taa? 22 Kwa maana hakuna neno lililostirika, illa kusudi lije likadhihirika; wala halikuwa siri, illa kusudi lije likatokea dhahiri. 23 Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie. 24 Akawaambia, Tafakarini msikialo, kipimo mpimacho mtapimiwa kile kile, na bado mtazidishiwa. 25 Kwa maana mtu aliye na kitu atapewa, nae asiye na kitu, hatta kile alicho nacho ataondolewa. 26 Akanena, Ufalme wa Mungu, mithili yake ni mtu aliyemwaga mbegu juu ya inchi: 27 akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikimea na kukua, asivyojua yeye. 28 Maana inchi huzaa yenyewe, kwanza jani, tena suke, kiisha nganu mpevu katika suke. 29 Hatta matunda yakiiva, marra aupeleka mundu kwa kuwa mavuno yamewadia. 30 Akanena, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? au tuutie katika mfano gani? 31 Ni kama punje ya kharadali ambayo, ipandwapo katika inchi, ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika inchi, 32 na ikiisha kupandwa, hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikifanya matawi makuhwa; hatta ndege za anga waweza kukaa chini ya uvuli wake. 33 Kwa mifano mingi ya namna hii alikuwa akisema nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kusikia; 34 wala pasipo mfano hakusema nao: akawaeleza wanafunzi wake mambo yote kwa faragha. 35 Siku ile ilipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu. 36 Wakawaacha makutano, wakamchukua vile vile katika chomho kile kile. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja nae. 37 Ikatokea dharuba kuu ya npepo, mawimbi yakapiga chombo hatta kikaanza kujaa maji. 38 Yeye mwenyewe alikuwa katika shetri, amelala juu ya mto: wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunapotea? 39 Akaamka: akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, tulia. Upepo nkakoma, kukuwa shwari kuu. 40 Akawaambia, Mbona mu waoga? Hamna imani bado? 41 Wakaingizwa na khofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, bassi, hatta upepo na bahari zamtii? |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania