Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKAINGIA tena katika sunagogi: na palikuwako huko mtu mwenye mkono umepooza:

2 wakamvizia kuona kwamba atampotiya siku ya sabato: wapate kumshitaki.

3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.

4 Akawaambia, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? kuokoa roho au kuua? Wakanyamaza.

5 Akawakazia macho pande zote kwa ghadhabu, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu. Nyosha mkono wako. Akaunyosha: mkono wake ukapona ukawa mzima kama wa pili:

6 marra wakaloka wale Mafarisayo, wakamfanyia shauri pamoja na Maherodiano jinsi ya kumwangamiza.

7 Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake, akaenda baharini. Watu wengi sana wakamfuata toka Galilaya, na toka Yahudi, na toka Yerusalemi,

8 na toka Idumaya, na ngʼambu ya Yardani, na pande za Turo na Sidon, mkutano mkuu, waliposikia khabari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda; wakamwendea.

9 Akawaambia wanafunzi wake ya kama chombo kidogo kikae karibu nae, kwa sababu ya makutano, wasije wakamsonga.

10 Maana aliponya wengi, hatta wote waliokuwa na misiba wakamrukia wapate kumgusa.

11 Na pepo wachafu, killa walipomwona, wahanguka mbele yake, wakalia wakinena, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.

12 Akawagombeza sana, wasimdhihirishe.

13 Akapanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea.

14 Akaweka thenashara, wapate kuwa pamoja nae, na kusudi awatume kukhubiri,

15 na wawe na mamlaka ya kufukuza pepo.

16 Na Simon akampa jina, Petro;

17 na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, akawapa jina, Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo,

18 na Andrea, na Filipo, na Bartolomayo, na Mattayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thaddayo na Simon Mkanani,

19 na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti.

20 Kiisha wakaingia nyumbani; makutano wakakusanyika tena, wao wenyewe wasiweze kula hatta mkate.

21 Jamaa zake walipopata khabari wakatoka kwenda kumkamata: maana walinena, Amerukwa na akili.

22 Waandishi walioshuka kutoka Yahudi wakanena, Ana Beelzebul, na kwa uwezo wa mkuu wa pepo awafukuza pepo.

23 Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumfukuza Shetani?

24 Na ufalme nkilitinika juu ya nafsi yake ufalme ule hauwezi kusimama;

25 na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba ile haiwezi kusimama.

26 Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake akafitinika, hawezi kusimama, bali ana kikomo.

27 Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.

28 Amin, nawaambieni, Dbambi zote watasamehewa wana Adamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;

29 bali mtu atakaemkufuru Roho Mtakatifu hana masamaha hatta milele; bali atakuwa ana dhambi ya milele;

30 kwa vile walivyonena, Ana pepo mchafu.

31 Wakaja mama yake na ndugu zake; wakasimama nje, wakamtuma mtu kumwita.

32 Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka; wakamwambia, Mama yako, na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.

33 Akawajibu, akinena, Mama yangu na ndugu zangu ni nani?

34 Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akanena, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu.

35 Kwa maana mtu ye yote atakaeyafanya mapenzi ya Mungu, huyu ndive ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo