Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu wa Yakobo na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka.

2 Hatta assubuhi mapema, siku ya kwanza ya sabato, wakaenda kaburini, jua lilipochomoza;

3 wakasemezana wao kwa wao, Nani atakaetufingirishia lile jiwe kutoka mlangoni mwa kaburi?

4 Hatta walipotazama, wakaona ya kuwa lile jiwe limekwisha kufingirishwa; nalo lilikuwa kubwa nmo.

5 Na wakiingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe: wakastaajabu.

6 Nae akawaambia, Msistaajabu; muamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa: amefufuka: bayupo hapa: patazameni pahali walipomweka.

7 Lakini enendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya: huko mtamwona, kama alivyowaambia.

8 Wakatoka humo, wakakimbia kutoka kaburini: kwa maana waliingia tetemeko na ushangao: wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa.

9 Alipofufuka Yesu assubuhi siku ya kwanza ya sabato alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambae kwamba alimtoa pepo saba.

10 Huyu akashika njia akawapa khabari wale waliokuwa pamoja nae tangu zamani, wangali wakiomboleza na kulia.

11 Na hawa waliposikia kama yu hayi akaonwa nae, hawakusadiki.

12 Baada ya haya akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba.

13 Na hawa wakaenda zao wakawapa khabari wale wengine: wala hawakuwasadiki hawa.

14 Baadae akaonekana na wale edashara walipokuwa wakila, akawalaumu kwa kutoamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki waliomwona alipofufuka.

15 Akawaambia, Enendem nlimwenguni mwote, mkaikhubiri injili kwa killa kiumbe.

16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

17 Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; Kwa jina langu watafukuza pepo; watasema kwa ndimi mpya;

18 watashika nyoka; hatta wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

19 Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.

20 Nao wakatoka, wakakhubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithubutishia neno kwa ishara zilizofuatana nalo. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo