Marko 15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 MARRA ilipokuwa assubuhi makuhani wakuu wakafanya shauri pamoja na wazee na waandishi na haraza zima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta kwa Pilato. 2 Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajihu, akamwambia, wewe unasema. 3 Makuhani wakamshitaki mengi. 4 Pilato akamwuliza tena akinena, Hujibu neno? Tazama mambo mangapi wanayokushitaki! 5 Wala Yesu hakujibu neno tena, hatta Pilato akataajabu. 6 Bassi katika siku kuu huwafungulia mfungwa mmoja, wamtakae. 7 Palikuwa na mtu aitwae Barabba, amefungwa pamoja na watu waliofanya fitina na kufanya uuaji katika fitina. 8 Makutano wakapaaza sauti zao, wakaanza kuomba vile kama alivvozoea kuwatendea. 9 Pilato akawajibu, akisema, Mnataka niwafungulie mfalme wa Wayahudi? 10 Kwa maana alifahamu ya kuwa makuhani wakuu wamemtoa kwa husuda. 11 Makuhani wakuu wakawataharakisha makutano, illi apende kuwafungulia Barabba. 12 Pilato akajibu tena akawaambia, Bassi wataka nimtendeni huyu mnenae kuwa Mfalme wa Wayahudi? 13 Wakapiga kelele tena, Msulibishe. 14 Pilato akawaambia, Kwani, ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, Msulihishe. 15 Pilato akapenda kuwafanyia radhi makutano, akawafungulia Barabba: akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, asulibiwe. 16 Askari wakamchukua ndani ya sebule, ndiyo Praitorio, wakakusanya pamoja kikosi kizima. 17 Wakamvika vazi jekundu, wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani; 18 wakaanza kumsalimu, Salamu Mfalme wa Wayahudi! 19 Wakampiga kichwa kwa unyasi, wakamtemea mate, wakapiga magoti, wakamsujudu. 20 Hatta wakiisha kumdhihaki, wakamvua lile vazi jekundu, wakamvika nguo zake mwenyewe; wakamchukua nje wamsulibishe. 21 Wakamtumikisha mtu aliyekuwa akipita, Simon Mkurene, akitoka mashamba, baba wa Iskander na Rufo, auchukue msalaba wake. 22 Wakamleta mahali palipokwitwa Golgotha, tafsiri yake, mahali pa kichwa. 23 Wakampa mvinyo iliyotiwa manemane anywe, nae hakupokea. 24 Wakamsulibi, wakagawanya nguo zake wakizipigia kura killa mtu atwae nini. 25 Ikawa saa tatu wakamsulibi. 26 Anwani ya mshitaka wake iliandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDU. 27 Na pamoja nae walisulibi wanyangʼanyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. 28 Bassi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na maasi. 29 Nao waliopita wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa vyao, wakisema, Ah! wewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, 30 jiponye nafsi yako, shuka msalabani. 31 Kadhalika na makuhani wakuu wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, Aliwaponya wengine; hawezi kujiponya nafsi yake. 32 Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Nao waliosulibiwa pamoja nae wakamlaumu, 33 Ilipokuwa saa sita, pakawa na giza juu ya inchi yote, hatta saa tissa. 34 Na saa tissa Yesu akapiga kelele kwa sauti kuu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? tafsiri yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? 35 Na baadhi yao waliohudhuria, wakisikia, wakasema, Anamwita Eliya. 36 Mtu akapiga mbio, akajaza sifongo siki, akaitia jim ya unyasi, akamnywesha, akisema, Acheni; na tuone kwamba Eliya anakuja kumshusha. 37 Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38 Pazia la patakatifu likapasuka vipande viwili toka juu hatta chini. 39 Bassi yule akida, aliyesimama akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa, Mwana wa Mungu. 40 Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; katika hawa alikuwa Mariamu Magdalene, na Mariamu mama wa Yakobo mdogo na wa Yose, na Salome: 41 hawa ndio waliomfuata alipokuwa Galilaya, na kumkhudumia; na wengine wengi waliopanda pamoja nae hatta Yerusalemi. 42 Hatta ikiisba kuwa jioni, kwa sababu ni Maandalio, ndiyo siku iliyo kabla ya sabato, 43 akaenda Yusuf, mtii wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza la mashauri, nae mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu. 44 Pilato akastaajabu, kwa sababu amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo. 45 Hatta alipokwisha kupata hakika, akamtunukia Yusuf maiti. 46 Akanunua saanda, akamshusha, akamfungia ile saanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani: akafingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi. 47 Mariamu Magdalene na Mariamu wa Yose wakapatazama alipowekwa. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania