Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BAADA ya siku mbili ilikuwa siku kuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa: makuhani wakuu na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.

2 Kwa maana walisema, Sio wakati wa siku kuu, isije ikawa fitina katika watu.

3 Nae akiwapo Bethania, nyumbani mwa Simon mwenye ukoma, ameketi chakulani, akaja mwanamke mwenye kibweta cha alabastro cha marhamu ya hali udi, safi, ya thamani nyingi; akakivunja kibweta cha alabastro akaimimina kichwani pake.

4 Palikuwa na watu waliochukiwa katika nafsi zao wakisema, Ya nini kupoteza marhamu namna hii?

5 maana marhamu hii ingalikuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi wakapewa maskini. Wakamnungʼunikia sana yule mwanamke.

6 Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamwudhi? amenitendea kazi njema:

7 maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi, na killa mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.

8 Ametenda alivyoweza; amenipaka mwili marhamu kwa ajili ya maziko yangu.

9 Amin, nawaamhieni, Killa ikhubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.

10 Yuda Iskariote, mmoja wa wathenashara, akaenda zake kwa makuhani wakuu, apate kumsaliti kwao.

11 Nao waliposikia wakafurahi, wakaahidi kumpa fedha. Akatafuta njia ya kumsaliti wakati wa kufaa.

12 Hatta siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja Pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Wapi unataka tuende tukaandalie uile pasaka?

13 Akapeleka wawili katika wanafunzi wake, akawaambia, nendeni zenu mjini; atakutana nanyi mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni:

14 na po pote atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu asema, I wapi sebule ya wageni, niile pasaka, pamoja na wanafunzi wangu?

15 Nae mwenyewe atawaonyesha orofa kuhwa, imetandikwa tayari: huko tuandalieni.

16 Wanafunzi wakatoka, wakaenda mjini, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka.

17 Ilipokuwa jioni yuaja pamoja na wathenashara.

18 Nao wakiisha kuketi chakulani, wakila, Yesu akasema, Amin, nawaambieni, mmoja wenu, nae anakula pamoja nami, atanisaliti.

19 Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia, mmoja mmoja, Ni mimi? na mwingine, Ni mimi?

20 Akawaamhia, Ni mmoja wa wathenashara, yeye achovyae pamoja nami katikakombe.

21 Kwa maana Mwana wa Adamu aenda zake kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu amesalitiwa nae: ingekuwa kheri kwake kama asingezahwa mtu yule.

22 Nao wakila, akatwaa mkate, akahariki, akamega, akawapa, akasema, Twaeni; huu ni mwili wangu.

23 Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote.

24 Akawaambia, Hii ni damu yangu, ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya watu wengi.

25 Amin, nawaambieni, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hatta siku ile nitakaponnywa mpya katika ufalme wa Mungu.

26 Wakiisha kuimba wakatoka kwenda mlima wa mizeituni.

27 Na Yesu akawaambia, Mtachukizwa nyote kwa ajili yangu nsiku huu: kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchunga, na kondoo watatawanyika.

28 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.

29 Petro akamwambia, Wajapochukizwa wote, lakini sio mimi.

30 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, Wewe leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo marra mbili, utanikana marra tatu.

31 Nae akazidi sana kusema, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana kabisa. Na wote wakasema vivi hivi.

32 Tena wakaja mahali jina lake Gethsemane; akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa muda nisalipo.

33 Akamchukua Petro na Yakobo na Yohana pamoja nae, akaanza kufadhaika sana na kuhangaika.

34 Akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa mkakeshe.

35 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomha, ya kuwa, ikiwezekana, saa hii impitie.

36 Akasema, Abba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikomhe hiki: walakini, si nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.

37 Akaenda akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Simon, umelala? Hukuweza kukesha saa moja?

38 Kesheni, kasalini, msipate kuingia majaribuni: roho ina nia njema, hali mwili dhaifu.

39 Akaenda zake fena, akaomha, akasema neno lili hili.

40 Hatta akaenda akawakuta wamelala tena, maana macho yao yanickuwa mazito, wala hawakujua la kumjibu.

41 Akaja marra ya tatu, akawaambia, Laleni sasa, hatta mwisho, kapumzikeni: yatosha, saa imekuja; Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi.

42 Ondokeni, twende; tazama, yeye anaenisaliti amekaribia.

43 Na alipokuwa katika kusema marra Yuda akafika, mmoja wa wathenashara, na pamoja nae mkutano, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu, na waandishi, na wazee.

44 Na yeye anaemsaliti amewapa ishara, akisema, Nitakaembusu, ndiye; mkamateni, mehukueni salama.

45 Alipokuja, marra akamwendea, akasema, Rabbi, Rabbi; akambusu sana.

46 Wakanyosha mikono yao wakamkamata.

47 Na mmoja wao waliohudhuria akavuta upanga, akampiga mtumwa wa kuhani mkuu, akamkata sikio.

48 Yesu akajibu, akawaambia, Kama juu ya mnyangʼanyi mmetoka na panga na marungu, kuja kunitwaa?

49 Killa siku nalikuwa mbele yenu bekaluni nikifundisha, wala hamkunikamata: lakini maandiko yapate kutimia.

50 Wote wakamwacha, wakakimbia.

51 Na kijana mmoja alimfuata, amejitanda nguo ya katani;

52 wakamkamata; nae akaiacha ile nguo ya katani, akawakimbia, yu uchi.

53 Wakamchukua Yesu kwa mkubani mkuu; wakamkusanyikia wote, makhani wakuu na wazee na waandishi.

54 Petro akamfuata mbali, hatta ndani katika behewa ya kuhani mkuu; akaketi pamoja na watumishi, anakota moto.

55 Makuhani wakuu na baraza wote wakatafuta ushuhuda juu ya Yesu wapate kumwua: wasione.

56 Kwa maana wengi walimshuhudia uwongo, na ushuhuda wao haukupatana.

57 Hatta watu wakasimama wakamshubudia kwa uwonoo, wakisema,

58 Sisi twalimsikia akiseina, Mimi nitaivunja hekalu hii iliyofanyika kwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga ingine isiyofanyika kwa mikono;

59 hatta hivi ushuhuda wao haukuwa sawa.

60 Kuhani mkuu akasimama kati kati, akamwuliza Yesu, akisema, Hujibu neno? Hawa wakushuhudiani?

61 Lakini akanyamaza, wala hakujibu neno. Knbani mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake aliye Mtukufu?

62 Yesu akasema, Mimi ndio yeye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbingu.

63 Kuhani mkuu akararua nguo zake, akisema, Tuna baja gani ya mashahidi wengine?

64 Mmesikia kufuru yake; mwaonaje? Wote wakamhukumu kuwa amepasiwa kufa.

65 Wengine wakaanza kumtemea mate, na kumfunika uso, na kumpiga konde, na kumwambia, Fanya unabii. Watumishi wakampiga makofi.

66 Na Petro alikuwa chini sebuleni, akaja mmoja wa vijakazi wa kuhani mkuu: akamwona Petro akikota moto;

67 akamtazama, akasema, Wewe nawe ulikuwa pamoja na yule Mnazareti, Yesu.

68 Akakana, akasema, Sijui wala si sikii usemavyo. Akatoka nje hatta ukumbini; jogoo akawika.

69 Na yule kijakazi akamwona tena, akaanza kuwaambia waliohudhuria, Huyu ni mmoja wao. Akakana tena.

70 Punde kidogo wale waliohudhuria wakamwambia Petro, Hakika u mmoja wao, kwa sababu u Mgalilaya wewe, na usemi wako kama usemi wao.

71 Akaanza kulaani na kuapiza, Simjui mtu huyu mnenae.

72 Jogoo akawika marra ya pili. Petro akalikumbuka neno lile aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo marra mbili, utanikana marra tatu. Na alipolifikiri, akalia.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo