Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, Mwalimu, namna gani ya mawe! namna gani ya majengo!

2 Yesu akajibu, akawaambia, Waona majengo haya makuhwa makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomelewa.

3 Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa mizeituni, kuelekea hekalu, Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea wakamwuliza kwa faragha, Tuambie, haya yatakuwa lini?

4 Na nini dalili ya wakati hayo yote yatakapokuwa karibu kutimia?

5 Yesu akajibu, akaanza kuwaambia, Jihadharini, mtu asiwadanganye; kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakinena,

6 Mimi ndiye: na watadanganya wengi.

7 Tena mtakaposikia vita na khabari za vita, msitishwe: maana hayana buddi kutukia, lakini mwisho wenyewe bado.

8 Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme utapigana na ufalme: kutakuwa na matetemeko ya inchi mahali mahali; kutakuwa na njaa, na fitina: Hayo ndio mwanzo wa utungu.

9 Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapelekeni maharazani: na katika masunagogi mtapigwa: na mtachukuliwa mbele za maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.

10 Tena sharti Injili ikhubiriwe kwanza katika mataifa yote.

11 Na watakapowachukueni, na kuwateni katika mikono ya watu, msianze kuwaza mtakayosema, wala msishughulike: lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni: kwa maana si ninyi mseniao, hali Roho Mtakatifu.

12 Na ndugu atamsaliti ndugu yake illi anawe, na baba mtoto wake, na watoto wataondoka jun ya wazazi wao, na kuwafisha.

13 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kustahimili hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.

14 Lakini mlionapo chukizo la uharibifu (lile lililoneuwa ua nabii Danieli) likisimama pasipolipasa (asomae na afahamu) ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani;

15 nae aliye juu ya dari asishuke nyumbani, wala asiingie kuchukua kitu katika nyumba yake,

16 Nae aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake.

17 Ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku zile!

18 Ombeni kukimbilia kwerm kusiwe wakati wa baridi.

19 Kwa maana siku zile zitakuwa na shidda jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hatta sasa, wala hazitakuwa kamwe.

20 Na kama Bwana asingalizikatiza siku zile, asingeokoka mtu aliye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku zile.

21 Na wakati huo mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko huko, msisadiki:

22 kwa maana wataondoka Makristo wa nwongo, na manabii wa uwongo, watatoa ishara na ajabu, wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wale wateule.

23 Bali ninyi mwe macho: nimekwisha kuwaonyeni yote mbele.

24 Lakini siku hizo baada ya shidda ile jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake,

25 na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika.

26 Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na nguvu nyingi na utukufu.

27 Ndipo atakapowatuma malaika zake na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa inchi hatta upande wa mwisho wa mbingu.

28 Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liauzapo kuwa laini, na kuchanua majani yake, mwajua ya kuwa karibu wakati wa bari:

29 kadhalika na ninyi, myaonapo haya yanatukia, fahamuni ya kuwa ni karibu milangoni.

30 Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita kabisa, hatta haya yote yapatapo kuwa.

31 Mbingu na inchi zitapita: maneno yangu hayatapita kamwe.

32 Lakini khabari ya siku ile na saa ile hakuna aijuae, hatta malaika walio mbinguni, wala Mwana, illa Baba.

33 Angalieni, kesheni, ombeni, kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwa.

34 Ni kana kwamba mtu mwenye kusafiri, ameacha nyumba yake, amewapa amri watumwa wake, na killa mtu kazi yake, amemwamuru bawabu akeshe.

35 Kesheni bassi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au usiku wa manane, au awikapo jogoo, an assubuhi:

36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.

37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia Wote, Kesheni.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo