Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA walipokaribia Yerusalemi karibu na Bethfage na Bethania, kukabili mlima wa Mizeituni, akawatuma wawili katilia wanafunzi wake, akawaambia,

2 Enendeni zenu hatta kile kijiji kinachowakahili. Katika kuingia ndani yake marra mtaona mwana punda amefungwa, asiyepandwa na mtu hado; mfungueni, kamleteni.

3 Na mtu akiwaambieni, Mbona mnafanya hivi? semeni, Bwana ana haja nae; na marra atampeleka hapa.

4 Wakaenda zao, wakamwona mwana punda amefungwa penye mlango, nje katika njia kuu, wakamfungua.

5 Baadhi ya watu waliosimama huko wakawaamhia, Mnafanyani mkimfungua mwana punda?

6 Wakawaambia kama Yesu alivyowaagiza.

7 Wakamletea Yesu yule mwana punda, wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake.

8 Watu wengi wakatandaza mavazi yao njiani, wengine wakakata matawi ya miti na kuyatandaza njiani.

9 Watu waliotangulia na wale waliofuata wakapaaza sauti zao, wakinena, Utuokoe sasa; amebarikiwa ajae kwa jina la Bwana;

10 umebarikiwa ufalme ujao kwa jina la Bwana, ufalme wa baba yetu Daud. Utuokoe sasa, wewe uliye juu.

11 Yesu akaingia Yerusalemi hatta ndani ya hekalu: na alipokwisha kutazama yote pande zote, kwa kuwa ni wakati wa jioni, akatoka akaenda Bethania pamoja na wathenashara.

12 Hatta assubuhi yake walipotoka Bethania akaona njaa.

13 Akaona toka mbali mtini wenye majani, akaenda illi labuda aone kitu juu yake: na alipofika hakuona kitu illa majani:

14 maana haukuwa wakati wa tini. Yesu akajibu, akauambia, Tangu leo hatta milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia.

15 Wakafika Yerusalemi, Yesu akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza watu waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadilio fedha, na viti vyao wauzao njiwa;

16 wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu.

17 Akafundisha, akiwaambia, Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali nanyi mmeifanya kuwa pango ya wanyangʼanyi.

18 Waandishi na makuhani wakini wakapata khabari wakatafuta jinsi ya kumwangamiza: maami walimwogopa, kwa sababu makutano yote walishangaa kwa elimu yake.

19 Na ilipokuwa jioni alitoka mjini.

20 Na assubuhi walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umekauka tangu shina lake.

21 Petro akakumbuka khabari yake, akamwabia, Rabbi, tazama, mtini ulioulaani umekauka.

22 Yesu akajibu, akamwambia, Mwe na imani kwa Mungu,

23 Amin, nawaambieni, Ye yote atakaenambia mlima huu, Ngʼoka ukatupwe baharini, asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yamekuwa, yatamtukia hayohayo aliyosema.

24 Kwa sababu biyo nawaambieni, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu.

25 Nanyi, killa msimamapo na kusali, sameheni, kama mkiwa na neno juu ya mtu: illi Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.

26 La, kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.

27 Wakafika Yerusalemi tena: hatta alipokuwa akitembea hekaluni, makuhani wakuu na waandishi na wuizee wakamwambia,

28 Kwa mamlaka gani utendayo haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya?

29 Yesu akajibu akawaambia, Mimi nami nitawauliza neno moja, nanyi nijibuni, kiisha nitawaambieni kwa mamlaka gani nitendayo haya.

30 Ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wana Adamu? Nijibuni.

31 Wakasemezana wao kwa wao, wakinena, Kama tukisema, Toka mbinguni, atasema, Mbona, bassi, hamkuniwamini?

32 Bali tukisema, Ulitoka kwa wana Adamu—waliogopa watu: maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii kweli kweli.

33 Wakamjibu Yesu, wakanena, Hatujui. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi kwa mamlaka gani nitendayo haya.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo