Marko 10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 AKAONDOKA huko akafika mipaka ya Yahudi kwa niia ya ngʼambu ya Yardani; watu wengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea. 2 Mafa risayo wakamwendea, wakamwuliza, Ni balali mtu kumwaeha mkewe? wakimjaribu. 3 Nae akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini? 4 Wakasema, Musa alitoa rukhusa kuandika khati ya talaka na kumwacha. 5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yemi aliwaandikia amri hii. 6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, Mungu aliwafanya mtu mume na mtu mke. 7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe: 8 na hawo wawili watakuwa mwili mmoja; hatta wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. 9 Bassi alivyoviunganisha Mungu, mwana Adamu asivitenganishe. 10 Hatta nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza khabari ya neno hilohilo. 11 Akawaambia, Killa mtu atakaemwacha mkewe na kuoa mwingine azini na kumkosa: 12 na mke, akimwacha mume wake na kuolewa na mtu mwingine, azini. 13 Wakamletea watoto wachanga illi awaguse: wanafunzi wake wakawakemea wao waliowaleta. 14 Lakini Yesu alipoona akachukiwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wachanga waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawo ufalme wa mbinguni ni wao. 15 Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali nfalme wa Mungu kama mtoto mchanga hatauingia kabisa. 16 Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki. 17 Hatta alipokuwa akitoka kwenda njiani mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele? 18 Yesu akamwambia, Mbona waniita mwema? hakuna mwema illa mmoja, ndiye Mungu. 19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudu uwongo, Usidanganye, Waheshimu haha yako na mama yako. 20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu ujana wangu. 21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate. 22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno lile, akaenda zake kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi. 23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Kwa shidda gani wenye mali wataingia katika ufalme wa Mungu! 24 Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, kwa shidda gani wenye kuitegemea mali wataingia katika ufalme wa Mungu! 25 Ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. 26 Nao wakashangaa mno, wakiambiana, Nani, bassi, awezae kuokoka? 27 Yesu akawakazia macho, akanena, Kwa wana Adamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu. 28 Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. 29 Yesu akajibu, akasema, Amin, nawaambieni, Hapana mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume au ndugu wake, au baba, au mama, au mke, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, au kwa ajili ya Injili, 30 illa atapewa marra mia sasa wakati huu, nyumba na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na mateso: na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. 31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho: na wa mwisho wa kwanza. 32 Wakawa njiani, wakipanda kwenda Yerusalemi; na Yesu alikuwa akiwatangulia: wakashangaa, na wakifuata wakaogopa. Akawachukua tena wale thenashara akaanza kuwaambia khabari za mambo yatakayompata, akinena, 33 Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemi: na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na waandishi, 34 na watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa mataifa, nao watamdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumtemea mate, na kumwua: na siku ya tatu atafufuka. 35 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, wakimwambia, Mwalimu, twataka utufanyie lo lote tutakalokuomba. 36 Akawaambia, Mwalaka niwafanyie nini? 37 Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto katika utukufu wako. 38 Yesu akawaambia, Hamjui mnaioliomba. Mnaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, na kubatizwa nbatizo nibatizwao mimi? 39 Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa: 40 bali khabari ya kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto sina amri kuwapeni, illa wao watapewa waliowekewa tayari. 41 Hatta wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana. 42 Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa majumbe wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. 43 Lakini haitakuwa hivi kwemi; bali mtu atakae kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mkhudumu wenu, 44 na mtu atakae kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. 45 Kwa maana Mwana wa Adamu nae hakuja kukhudumiwa bali kukhudumu, na kutoa roho yake iwe dia ya wengi. 46 Wakafika Yeriko: hatta alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka. 47 Aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, akaanza kupaaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daud, Yesu, unirehemu. 48 Yesu akasimama akaagiza aitwe. 49 Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; ondoka, anakuita. 50 Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. 51 Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyieni? Yule kipofu akamwambia, Rabbi, nipate kuona tena. 52 Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Marra akapata kuona tena; akafuata Yesu njiani. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania