Marko 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu; 2 kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Angalia, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, Atakaefanyiza njia yako mbele yako. 3 Sauti yake aliae jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake. 4 Akatokea Yohana, akibatiza jangwani, na kuukhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. 5 Wakamwendea inchi yote ya Yahudi, nao wa Yerusalemi, wakabatizwa nae katika mto Yardani, wakiziungama dhambi zao. 6 Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kimioni mwake, akila nzige na asali ya mwitu. 7 Akakhubiri akinena, Yuaja nyuma yangu aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba sistabili kuinama na kuzifungua kanda za viatu vyake. 8 Mimi naliwabatizeni kwa maji; bali yeye atawabalizeni kwa Roho Mtakatifu. 9 Tena, siku zile, alikuja Yesu kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yardani. 10 Marra akapanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kwa mfano wa hua, akishuka juu yake; 11 sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwana wangu mpendwa, ndiwe unipendezae. 12 Marra Roho akamwongoza hatta jangwani. 13 Akawako huko jangwani siku arubaini, akijaribiwa na Shetani; nae alikuwa pamoja na nyama wakali, na malaika walikuwa wakimkhudumia. 14 Hatta baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiikhubiri injili ya ufalme wa Mungu, 15 akineua, Wakati umetimia, na ufalme wa Muugu umekaribia; tubuni, kaiaminim injili. 16 Nae akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simon na Andrea ndugu yake, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. 17 Yesu akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. 18 Marra wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. 19 Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake, nao pia walikuwa chomboni, wakizitengeneza nyavu zao. 20 Marra akawaita: wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya chombo pamoja na watu wa mshahara, wakaenda, wakamfuata. 21 Wakashika njia hatta Kapernaum; na siku ya sabato akaingia sunagogi, akafundisha. 22 Wakashangaa kwa mafundisho yake; kwa sababu alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka wala si kama waandishi. 23 Palikuwapo katika sunagogi yao mtu mwenye pepo mchafu; akapaaza sauti, 24 akinena, Tʼuna nini nawe, Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu. 25 Yesu akamkaripia, akinena, Fumba kinywa, umtoke. 26 Yule pepo mchafu akamrarua, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. 27 Wakashangaa wote hatta wakaulizana, wakinena, Nini hii? Elimu hii mpya ni elimn gani? Maana kwa mamlaka awaamuru pepo wachafu nao wakamtii! 28 Khahari zake zikaenea marra inchi zote kando ya Galilaya. 29 Marra walipotoka katika sunagogi, wakalika nyumbani kwa Simon na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana. 30 Mama wa mkewe Simon alikuwa kitandani, hawezi homa; 31 marra wakamwambia khahari zake: akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawakhudumia. 32 Hatta ilipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, wakamletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo. 33 Na mji wote nlikuwa umekusanyika mlangoni. 34 Akaponya wengi waliokuwa na maradhi nyingine nyingine, akafukuza pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua. 35 Hatta alfajiri na mapema sana, akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipo watu akasali huko. 36 Simon ua wenziwe wakamfuata; 37 wakamwona, wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. 38 Akawaambia, Twende pengine hatta vijiji vilivyo karibu, nipate kukhubiri na huko; maana kwa hiyo nalitokea. 39 Akawa akikhubiri katika masuuagogi yao, katika inchi yote ya Galilaya, na kufukuza pepo. 40 Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa. 41 Yesu akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika. 42 Marra hiyo ukoma wake ukamwondoka, akatakasika. 43 Akamkataza kwa nguvu, marra akamwondosha, akamwambia, Fahamu, usimpe khabari mtu ye yote, 44 bali enenda zako ukajiouyeshe kwa kuhani ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, illi kuwa ushuhuda kwao. 45 Nae akatoka, akaanza kukhubiri mengi, na kulitangaza lile neno, hatta Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwa nje mabali pasipo watu; wakamwendea kutoka killa pahali. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania