Luka 9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 AKAWAITA wale thenashara akawapa uweza na mamlaka juu ya pepo wote, na kuponya maradhi. 2 Akawatuma kuukhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 3 Akawaambia, Msichukue kitu cha njiani, fimbo wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala msiwe na kanzu mbili. 4 Na nyumba yo yote mtakayoingia, kaeni humo, katokeni humo. 5 Na wo wote wasiowakarihisheni, mtokapo katika mji ule, yakungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu illi kuwa ushuhuda juu yao. 6 Wakaenda zao, wakazunguka katika vijiji, wakiikhubiri injili, na kuponya watu killa pahali. 7 Hatta Herode tetrarka akasikia yote yaliyotendwa nae, akaona mashaka, kwa kuwa wengine walisema kwamba Yohana amefufuka katika wafu: 8 na wengine kwamba Eliya ametokea: na wengine kwamba nabii mmoja katika wale wa kale amefufuka. 9 Herode akasema, Yohana nimemkata kichwa: bassi, nani huyu ambae ninasikia khabari zake za namna hii? Akatafuta kumwona. 10 Wale mitume waliporudi wakamweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda zake kwa faragha mahali pasipo watu, karibu na mji uitwao Bethsaida. 11 Namakutano walipojua wakamfuata: akawakaribisha, akanena nao khabari za ufalme wa Mungu, akawaponya waliokuwa na haja ya kuponywa. 12 Hatta jua lilipoanza kuchwa wale thenashara wakamwendea wakamwambia, Uwaage makutano illi waende zao hatta vijiji vilivyo kandokando na mashamba wakapate mahali pa kulala na vyakula: maana hapa tulipo nyika tupu. 13 Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakasema, Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki mbili, tusipokwenda sisi wenyewe tukawannnulie vyakula watu hawa wote. 14 Kwa maana walikuwako wanaume wapata elfu tano. 15 Akawaambia wanafunzi wake, Waketisheni watu kwa safu, killa safu watu khamsini. 16 Wakafanya hivi, wakawaketisha wote. Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi, kuviweka mbele ya makutano. 17 Wakala, wakashiba wote: na vile vipande vilivyowabakia vikaokotwa, vikapu thenashara. 18 Ikawra alipokuwa akisali peke yake wanafunzi wake walikuwa pamoja nae: akawanliza, akisema, Makutano huninena mimi kuwa nani? 19 Wakajibu, wakasema, Yohana Mbatizaji: na wengine, Eliya: na wengine kwamba nabii mmoja katika wale wa kale amefufuka. 20 Akawaambia, Na ninyi mwaninena mimi kuwa nani? 21 Petro akajibu, akasema, Kristo wa Mungu. 22 Akawaagiza na kuwaamuru wasimwambie mtu neno hili, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. 23 Akawaamhia wote, Atakae kuniandama, na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake killa siku, anifuate. 24 Kwa maana mtu akitaka kuisalimisha roho yake ataiangamiza, nae atakae kuitoa roho yake kwa ajili yangu, huyu ataisalimisha. 25 Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote na kujipoteza, au kupata khasara ya roho yake? 26 Kwa sababu killa mtu atakaenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya huyo atakapokuja katika utukufu wake, na wa Baba yake, na wa malaika watakatifu. 27 Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataionja mauti kabisa hatta watakapouona ufalme wa Mungu. 28 Hatta baada ya maneno haya, panapo siku nane, akamchukua Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani kusali. 29 Ikawa alipokuwa akisali, sura ya uso wake ikageuka, na mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta. 30 Na tazama, watu wawili walikuwa wakisemezana nae, nao ni Musa na Eliya, 31 walioonekana katika utukufu, wakanena khahari ya kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemi. 32 Petro, nao waliokuwa pamoja nae, walikuwa wamelemewa sana na usingizi: lakini walipokwisha kuamka wakauona utukufu wake, na wale watu wawili, waliosimama pamoja nae. 33 Ikawa hawo walipokuwa wakijitenga nae, Petro akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa: na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, kimoja cha Eliya: nae hajui asemalo. 34 Hatta alipokuwa akisema haya likawako wingu, likawatia uvuli; wakaogopa walipoingia katika lile wingu. 35 Sauti ikatoka katika lile wingu ikasema, Huyu ni Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. 36 Na sauti hii ilipokuja Yesu akaonekana peke yake. Nao wakanyamaza wasimwambie mtu siku zile neno lo lote la hayo waliyoyaona. 37 Ikawa siku ya pili yake, waliposhuka mlimani, mkutano mkuu wakakutana nae. 38 Na tazama, mtu mmoja katika ule mkutano akapaaza sauti yake, akisema, Mwalimu, nakuomha, mwangalie mwanangu, kwa kuwa yeye ni mwanangu pekee; 39 na tazama, pepo humshika, nae marra hulia; tena humrarua, akatoka povu, wala hamtoki illa kwa shidda, akimchubuachubua. 40 Nikawaomba wanafunzi wako wamfukuze, wasiweze. 41 Yesu akajibu akasema, Enyi kizazi kisichoamini na upofu, nikae nanyi hatta hui? Mlete mwana wako hapa. 42 Alipokuwa katika kumwendea, yule pepo akambwaga akamraruararua. Yesu akamkaripia yule pepo mchafu, akamponya yule mtoto, akamrudishia baba yake. 43 Watu wote wakashangaa kwa adhama yake Mungu. Hatta wote walipokuwa wakistaajabia mambo yote aliyoyafanya akawaambia wanafunzi wake, 44 Yawekeni maneno haya masikioni mwenu: kwa maana Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu. 45 Lakini hawakulifuhamu neno lile, likawa limefichwa kwao wasipate kulitambua. Wakaogopa kumwuliza maana ya neno lile. 46 Yakawaingia mabishano, ni nani atakaekuwa mkubwa miongoni mwao. 47 Nae Yesu alipoona mawazo ya mioyo yao, akatwaa kitoto akamweka karibu yake, 48 akawaambia, Killa mtu atakaempokea kitoto hiki kwa jina langu, anipokea mimi, na killa mtu atakaenipokea mimi, ampokea yeye aliyenituma. Maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu ninyi nyote, huyu atakuwa mkubwa. 49 Yohana akajibu, akasema, Mwalimu, tulimwona mtu anafukuza pepo kwa jina lako, tukamkataza kwa kuwa hatufuati sisi. 50 Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa maana yeye asiye kinyume chetu ni upande wetu. 51 Ikawa siku za kupandishwa kwake juu zilipokuwa karibu kutimia, yeye mwenyewe akauelekeza nso wake kwenda Yerusalemi. 52 Akatuma wajumbe mbele ya uso wake, wakashika njia, wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, illi kumfanyia tayari. 53 Nao hawakumkaribisha, kwa sababu nso wake ameuelekeza kwenda Yerusalemi. 54 Wanafunzi wake Yokobo na Yohana walipoona haya, wakasema, Bwana, wataka tuambie moto ushuke kutoka mbinguni uwaangamize, kama na Eliya alivyofanya? 55 Akageuka, akawakaripia, akasema, Hamjui ni moyo wa namna gani mlio nao. 56 Maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za wana Adamu, bali kuziokoa. Wakaenda zao hatta mji mwingine. 57 Na walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja akamwambia, Nitakufuata ko kote uendako, Bwana. 58 Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vioto vyao, bali Mwana wa? Adamu hana pa kujilaza kichwa chake. 59 Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe rukhusa niende kwanza, nikamzike baba yangu. 60 Akamwambia, Waache wafu wazike wafu wao, bali wewe enenda zako ukautangaze ufalme wa Mungu. 61 Na mwingine nae akasema, Nitakufuata, Bwana, lakini kwanza nipe rukhusa nikawaage watu wa nyumbani mwangu. 62 Yesu akamwambia, Hakuna mtu aliyetia mkono wake alime, khalafu akatazama nyuma, afaae kwa ufalme wa Mungu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania