Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 IKAWA muda si muda alikuwa akizungukazunguka katika miji na vijiji, akikhutubu na kukhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu. Na wale thenashara walikuwa pamoja nae,

2 na wanawake kadha wa kadha waliokuwa wameponywa pepo wabaya na magonjwa, Mariamu aliyeitwa Magdalene, aliyetokwa na pepo saba,

3 na Joanna mkewe Kuza waklli wake Herode, na Susanna, na wengine wengi, waliokuwa wakimkhudumia kwa mali zao.

4 Makutano mengi yalipokutanika, na watu wa killa mji wakimjia, akasema kwa mfano:

5 Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda, nyingine zikaanguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege za anga wakazila.

6 Nyingine zikaanguka penye mwamba, zikamea, zikakauka kwa kukosa maji.

7 Nyingine zikaanguka kati ya miiba, nayo miiba ikamea pamoja nazo, ikazisonga.

8 Nyingine zikaanguka penye udongo mwema, zikamea, zikazaa mia mia. Alipokuwa akinena haya, akapaaza sauti yake, akisema, Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.

9 Wanafunzi wake wakamwuliza, wakinena, Mfano huu ni nini?

10 Akasema, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mungu, bali wengineo kwa mifano, illi wakiona, wasione, na wakisikia, wasitambue.

11 Na mfano ndio huu: Mbegu ni neno la Mungu.

12 Na wale wa njiani, ndio wasikiao, ndipo huja Shetani na kulitoa lile neno mioyoni mwao, illi wasije wakaamini, wakaokoka.

13 Na wale juu ya mwamba ndio wale ambao, walisikiapo neno, hulipokea kwa furaha; na hawa hawana mizizi, huamini kwa kitambo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.

14 Nazo zilizoangukia miibani, hawa ndio waliosikia, nao wakienda zao husongwa na shughuli, na mali, na anasa za maisha, wasizae kwa utimilifu.

15 Nazo penye udongo mwema, hawa ndio ambao kwamba kwa moyo mzuri na mwema hulisikia neno, wakalishika, wakazaa kwa saburi.

16 Hakuna mtu awashae taa na kuifunika kwa chombo au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kibao cha kuwekea faa, illi waingiao wauone mwanga.

17 Kwa maana hakuna neno lililostirika ambalo halitakuwa dhabiri, wala neno lililofichwa ambalo halitajulikana, na kutokea wazi.

18 Jihadharini, bassi, jinsi msikiavyo. Maana yeye aliye na kitu, atapewa: nae asiye na kitu ataondolewa hatta kitu kile ambacho anaonekana kuwa anacho.

19 Mama yake na ndugu zake wakamwendea wala hawakuweza kumkaribia kwa sababu ya mkutano.

20 Akapewa khabari na watu, waliosema, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kukuona.

21 Lakini yeye akajibu akawaambia, Mama yangu na ndugu zangu ndio hawa walisikialo neno la Mungu na kulitenda.

22 Ikawa siku mojawapo ya siku zile akapanda chomboni, yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu ya ziwa: wakatweka matanga.

23 Na walipokuwa wakienda kwa matanga akalala usingizi. Ikashuka dharuba ya upepo juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika khatari.

24 Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Mwalimu, Mwalimu, tunaangamia. Akaondoka, akaukemea upepo, na msukosuko wa maji, vikakoma, kukawa shwari.

25 Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakastaajabu, wakasemezana, Huyu ni nani, bassi, kwa kuwa hatta upepo na bahari aviamuru vikamtii?

26 Wakashuka pwani katika inchi ya Wagadareni, inayokabili Galilaya.

27 Hatta aliposhuka pwani, alikutwa na udu mmoja wa mji ule, aliyekuwa ua pepo siku nyingi, nae kwa muda mrefu alikuwa havai nguo, wala hakai nyumbani illa makaburini.

28 Alipomwona Yesu, akapiga kelele, akamwangukia, akasema kwa sauti kuu. Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuomba usiniadhibu.

29 Kwa sababu amemwamuru yule pepo mchafu kumtoka mtu yule. Maana marra nyingi amempagaa, nae akafungwa, akilindwa, na kufungwa minyororo na pingu, akavikata vile vifungo, akafukuzwa na yule pepo hatta jangwani.

30 Yesu akamwuliza, akisema, Jina lako nani? Akasema, Legioni, kwa sababu pepo wengi wamemwingia.

31 Akamsihi asiwaamuru waende zao hatta abusso.

32 Na kulikuwako kundi la nguruwe wengi, wakilisha mlimani. Wakamsihi awape rukhusa kuwaingia wao.

33 Akawapa rakhusa: wale pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, lile kundi likatelemka kwa kassi gengeni, wakafa baharini.

34 Wachungaji walipoona, wakakimbia, wakaenda zao wakaeneza khabari mjini na mashambani.

35 Wakatoka waone khabari iliyotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mtu aliyetokwa na wale pepo ameketi migunni pa Yesu, amevaa nguo, ana akili zake: wakaogopa.

36 Nao walioona wakawaeleza jinsi yule mwenye pepo alivyoponywa.

37 Na watu wote wa inchi ya Wagadarene iliyo kando kando wakamwomba aondoke kwao, kwa sababu walishikwa na khofu nyingi; bassi akakiingia chombo akarudi.

38 Na yule mtu aliyetokwa na pepo akamsihi awe pamoja nae: lakini Yesu akamwaga, akisema,

39 Rudi nyumbani kwako, ukayakhubiri mambo makuu aliyokutendea Mungu. Akaenda zake, akikhubiri katika mji mzima mambo makuu ambayo Yesu amemtendea.

40 Yesu alipokuwa akirudi makutano wakamkaribisha, kwa maana watu wote walikuwa wakimngojea.

41 Na tazama, mtu mmoja jina lake Yairo akamjia: nae alikuwa mkuu wa sunagogi: akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani mwake:

42 kwa sababu ana binti, mwana wa pekee, umri wake amepata miaka thenashara, nae yu katika kufa. Na katika kwenda kwake makutano wakamsonga.

43 Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu tangu miaka thenashara, aliyegharimu vitu vyote alivyo navyo akawapa tabibu asipate kuponywa na mtu aliye yote,

44 akamwendea kwa nyuma, akamgusa upindo wa nguo yake, marra kukakoma kule kutoka damu kwake.

45 Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Bassi watu wote walipokana, Petro nao walio pamoja nae wakamwambia, Bwana, Makutano wanakuzunguka na kukusonga, nawe unasema, Ni nani aliyenigusa?

46 Yesu akasema, Mtu alinigusa, kwa kuwa naliona nguvu zimenitoka.

47 Yule mwanamke alipoona ya kuwa hakustirika, akaja akitetemeka, akamwangukia, akamweleza mbele ya watu wote sababu hatta akamgusa, na jinsi alivyoponywa marra moja.

48 Akamwambia. Jipe moyo mkuu, binti, imani yako imekuponya; enenda zako kwa amani.

49 Alipokuwa akinena haya, mtu akaja, ametoka kwa yule mkuu wa sunagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha kufa, usimsumbue mwalimu.

50 Yesu aliposikia, akamjibu, akasema, Usiogope, amini tu, nae ataokolewa.

51 Alipofika nyumbani, hakumwacha mtu aingie pamoja nae, illa Petro, na Yakobo na Yohana, na baba yake yule kijana na mama yake. Na watu wote walikuwa wakilia, wakimwombolezea.

52 Akasema, Msilie; kwa maana hakufa, bali amelala usingizi.

53 Wakamcheka sana, wakijua ya kuwa amekwisha kufa.

54 Nae akawatoa nje wote, akamshika mkono wake, akapaaza sauti yake, akisema, Kijana, ondoka.

55 Roho yake ikarudi, akasimama marra moja. Akaagiza apewe chakula.

56 Wazazi wake wakastaajabu sana, akawaamuru wasimwambie mtu lililotukia.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo