Luka 7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 ALIPOKWISHA kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu akaingia Kapernaum. 2 Na mtumishi wa akida mmoja alikuwa hawezi, karibu kufa, nae ni mtu aliyependwa nae sana. 3 Aliposikia khabari za Yesu akatuma baadhi ya wazee wa Wayahudi kwake, akimwomba aje, amwokoe mtumishi wake. 4 Nao walipolika kwa Yesu, wakamsihi kwa jubudi wakisema, 5 ya kama, Astahili umtendee neno hili, maana apenda taifu letu, nae alitujengea sunagogi letu. 6 Bassi Yesu akaenda pamoja nao. Hatta alipokuwa si mbali ya nyumba yake, yule akida akatuma rafiki kwake akimwambia, Bwana, usijisumbue, 7 maana si stahili yangu wewe uingie chini ya dari yangu: kwa biyo nalijiona sistahili kuja kwako: lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. 8 Sababu mimi nami ni mtu aliyewekwa chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda: na huyu, Njoo, huja; na mtumishi wangu, Fanya hivi, hufanya. 9 Yesu aliposikia haya akamstaajabia akawageukia makutano waliokuwa wakimfuata, akisema, Nawaambieni, Hatta katika Israeli sikuona imani nyingi namna hii. 10 Bassi wale waliotumwa waliporudi nyumbani kwake, wakamkuta yule mtumishi, aliyekuwa hawezi, yu mzima. 11 Ikawa khalafu yake, akaenda mji uitwao Nain, wanafunzi wake na watu wengi wakafuatana nae. 12 Bassi, alipokaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, mwana pekee wa mama yake, nae mjane; na watu wa mji wengi pamoja nae. 13 Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie. 14 Akaenda karibu, akaligusa jeneza; wale wachukuzi wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Ondoka. 15 Yule maiti akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. 16 Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake. 17 Zikatoka hizo khabari zake katika Yahudi yote, na katika inchi yote iliyozunguka. 18 Bassi wanafunzi wake Yohana wakamwarifu haya yofe. 19 Yohana akaita wawili katika wanafunzi wake akawapeleka kwa Yesu, akisema, Wewe ndiye yule ajae, au tumtazamie mwingine? 20 Bassi watu hawo walipofika kwake wakasema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiye ajae au tumtazamie mwingine? 21 Saa ileile akawaponya watu wengi maradhi zao, na misiba yao, na pepo wabaya: na vipofu wengi akawakarimia kuona. 22 Akajibu, akawaambia, Enendeni, mkamweleze Yohana mliyoyaona na kuyasikia: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanakhubiriwa khahari njema: 23 na yu kheri ye yote asiyechukizwa nami. 24 Na wale wajumbe wa Yohana, walipokwisha kwenda zao, akaanza kuwaambia makutano khabari za Yohana, Mlitoka kwenda jangwani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? 25 Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi meroro? Fahamuni, watu wenye nguo za umalidadi na kuishi maisha ya anasa wamo katika majumba ya wafalme. 26 Bali mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambieni, na aliye zaidi ya nabii. 27 Huyu ndiye aliyeandikiwa, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako atakaeitengeneza njia yako mbele yako. 28 Maana nawaambieni, Katika wazao wa wanawake hapana nabii aliye mkuu kuliko Yobana Mbatizaji: lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye. 29 Watu wote na watoza ushuru waliposikia wakampa Mungu haki, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana. 30 Bali Mafarisayo na wana sharia walijikatalia shauri la Mungu kwa kuwa hawakubatizwa nae. 31 Bwana akasema, Nitawafananisha na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini? 32 Wamefanana na watoto, waketio sokoni, wakiitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi nanyi hamkucheza, tuliomboleza, nanyi hamkulia. 33 Kwa maana Yohana Mbatizaji amekuja, hali mkate, wala hanywi divai, mkasema, Yuna pepo. 34 Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, mkasema, Mlafi huyu, na mnywaji wa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi. 35 Na hekima imepata haki yake kwa watoto wake wote. 36 Mtu mmoja katika Mafarisayo akamtaka ale chakula pamoja nae. Akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. 37 Kumbe! Mwanamke mmoja katika mji ule ahyekuwa mwenye dhambi, alipopata khabari ya kuwa ameketi katika nyumba ya yule Farisayo, akaleta chupa cha alabastro yenye marhamu, 38 akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumchuruzia miguu kwa machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake akibusu sana miguu yake, na kuipaka yale marhamu. 39 Yule Farisayo aliyemwalika, alipoona haya akasema kimoyomoyo, akinena, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angalimjua huyu ni nani! na ni mwanamke gani anaemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi. 40 Yesu akajibu akamwambia, Simon, nina neno la kukuambia. Akanena, Mwalimu, sema. 41 Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili: mmoja aliwiwa nae dinari khamsi mia, na wa pili khamsini. 42 Nao wakiwa hawana kitu cha kulipa, akawasamehe wote wawili. Bassi, sema, Katika hawo ni nani atakaempenda zaidi? 43 Simon akajibu akasema, Nadhani ni yule aliyesamehewa nae mengi. Akamwambia, Umehukumu haki. 44 Akamgenkia yule mwanamke, akamwambia Simon, Wamwona mwanamke huyu? Naliingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawia miguu, bali huyu amenichuruzia miguu kwa machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. 45 Hukunibusu: bali huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu. 46 Hukunipaka kichwa changu mafuta: bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. 47 Kwa ajili hiyo, nakuambia, Amesamehewa dhambi zake zilizo nyingi kwa kuwa amependa sana. Nae asamehewae kidogo hupenda kidogo. 48 Akamwambia, Umesamehewa dhambi zako. 49 Na wale walioketi pamoja nae wakaanza kusema ndani ya mioyo yao, Nani huyu hatta akasamehe dhambi? 50 Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa; enenda zako kwa amani. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania