Luka 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 IKAWA makutano walipomsonga, wakisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa akisimama kando ya ziwa la Genesareti: 2 akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa: na wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao. 3 Akaingia chombo kimoja, kilichokuwa cha Simon, akamtaka asogeze kidogo kutoka pwani. Akakaa, akawafundisha makutano katika chombo. 4 Alipokwisha kusema, akamwambia Simon, Sogea hatta kilindini, mkashushe nyavu zenu kwa uvuvi. 5 Simon akajibu, akasema, Bwana, tulisumbuka usiku kucha, tusipate kitu: illakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. 6 Bassi, walipofanya hivi, wakakusanya wingi wa samaki: nyavu zao zikaanza kukatika. 7 Wakawaashiri wenzi wao katika chombo cha pili, waje kuwasaidia. Wakaenda wakavijaza vyombo vyote viwili, hatta kuvizamisha. 8 Simon Petro alipoona haya, akaanguka magotini pa Yesu, akasema, Toka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana. 9 Kwa maana ushangao umemshika yeye, na wote waliokuwako pamoja nae, kwa uvuvi wa samaki walioupata. 10 Kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washiriki wa Simon, Yesu akamwambia Simon, Usiogope; tangu sasa utakuwa ukivua watu. 11 Na walipoleta vyombo pwani, wakaacha vyote wakamfuata. 12 Ikawa alipokuwa katika mji mmoja wa miji ile, tazama, palikuwa na mtu amejawa ukoma; nae alipomwona Yesu, akaanguka kifudifudi, akamwomba, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. 13 Nae akauyosha mkono wake, akamgusa, akinena, Nataka; takasika. Marra ukoma wake ukamwounoka. 14 Akamwagiza asimwambie mtu: illa enenda, ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe kwa kutakasika kwako alivyoamuru Musa, illi kuwa ushuhuda kwao. 15 Lakini khabari zake zikazidi kuenea, wakakutana makutano mengi kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. 16 Lakini yeye alikuwa akijitenga jangwani na kusali. 17 Hatta siku moja ya siku zile alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waandishi wameketi, waliokuwa wametoka katika killa kijiji cha Galilaya, na cha Yahudi, na Yerusalemi; uweza wa Bwana ulikuwa pamoja nae apate kuwaponya. 18 Na kumbe! watu wanachukua mtu kitandani mwenye kupooza: wakitaka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake. 19 Hatta walipokosa pa kumpeleka ndani kwa sababu ya lile kundi la watu, wakapanda juu ya dari wakampisha katika matofali, wakamshusha na kitanda chake hatta katikati mbele ya Yesu. 20 Alipoona imani yao, akamwambia, Ee mtu, dhambi zako zimeondolewa. 21 Wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kutafakari wakanena, Nani huyu anaesema kufuru? Nani awezae kuondoa dhambi, isipokuwa mmoja ndiye Mungu? 22 Yesu akafahamu fikara zao akajibu, akawaambia, Mnafikiri nini mioyoni mwenu? 23 Vipi vyepesi, kusema, Dhambi zako zimeondolewa, au kusema, Ondoka, ukaende. 24 Lakini mpate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani ya kuondoa dhambi (alimwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako ukaende nyumbani kwako. 25 Marra akasimama mbele yao, akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani kwake, akimhimidi Mungu. 26 Ushangao ukawashika wote wakamtukuza Mungu: wakajaa khofu, wakinena, Tumeona maajabu leo. 27 Baada ya haya akatoka, akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, amekaa forodhani, akamwambia, Nifuate. 28 Akaacha vyote akaondoka akamfuata. 29 Nae Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake: na palikuwa na kundi kubwa la watoza ushuru, na watu wengine waliokuwa wameketi pamoja nao chakulani. 30 Mafarisayo na waandishi wao wakawanungʼunikia wanafunzi wake, wakisema, Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? 31 Yesu akajibu, akawaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi: 32 sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu. 33 Nao wakamwambia, Kwa nini wanafunzi wa Yohana wanafunga marra nyingi na kusali, na wanafunzi wa Mafarisayo wanafanya vilevile, bali wanafunzi wako hula na hunywa? 34 Yesu akawaambia, Je! mwaweza kuwafungislia wana wa arusi, maadam Bwana arusi yupo pamoja nao? 35 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa Bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile. 36 Akawaambia mithali, Hakima apasuae kiraka cha nguo mpya na kukitia katika vazi kuukuu: ikiwa atia aipasua ile mpya, na kile kiraka cha nguo mpya hakilingani na lile vazi kuukuu. 37 Wala hakuna mtu atiae divai mpya katika viriba vikuukuu: ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua vile viriba, divai yenyewe ikamwagika, viriba vikapotea. 38 Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya. 39 Wala hakuna mtu anywae divai ya kale, marra akatamani divai mpya, maana asema, Ile ya kale ni njema zaidi. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania