Luka 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NA Yesu, akijaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani: akaongozwa na Roho kwenda jangwani, akijaribiwa na Shetani muda wa siku arubaini. 2 Na siku zile hakula kitu; hatta zilipotimia, akaona njaa. 3 Shetani akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. 4 Yesu akamjibu, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, hali kwa killa neno la Mungu. 5 Shetani akampandisha juu ya mlima mrefu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Shetani akamwambia, Nitakupa mamlaka haya yote, na fakhari yake: kwa kuwa nimekabidhiwa, nami nampa ye yote nimtakae: 7 bassi, wewe ukisujudu mbele yangu, yote yatakuwa yako. 8 Yesu akamwambia, Nenda zako nyuma yangu, Shetani: maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu. 9 Akamwongoza hatta Yerusalemi, akamweka juu ya ukumbi wa hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini, toka huku: 10 maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde, 11 na, Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako kalika jiwe. 12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. 13 Hatta alipomaliza killa jaribu Shetani akaondoka kwake kwa muda. 14 Yesu akarudi kwa nguvu za Roho hatta Galilaya, khabari zake zikaenea katika inchi yote iliyo kando kando. 15 Nae alikuwa akifundisha katika masunagogi yao, akitukuzwa na watu wote. 16 Akaenda Nazareti, mahali alipokuwa amelelewa: akaingia katika sunagogi siku ya sabato, kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama illi asome. 17 Akapewa chuo cha nabii Isaya: bassi alipokwisha kukifunua chuo hicho, akapaona pahali palipoandikwa, 18 Roho ya Bwana ni juu yangu, Kwa sababu amenitia mafuia kuwakhubiri maskini khabari njema. Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo, Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa, na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha wa huru waliosetwa, 19 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20 Akakifunga chuo, akampa mkhudumu, akaketi: watu wote waliokuwa katika sunagogi wakamkazia macho. 21 Akaanza kuwaambia, Leo andiko hili limetimia masikioni mwenu. 22 Wakamshuhudia wote, wakayastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake: wakanena, Huyu siye Mwana wa Yusuf? 23 Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia methali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako: mambo yote tuliyosikia yametendeka Kapernaum, yatende na hapa pia katika inchi yako mwenyewe. 24 Akawaambia, Amin, nawaambieni, Hapana nabii apatae kukubaliwa katika inchi yake mwenyewe. 25 Lakini kwa kweli nawaambieni, Palikuwa wajane wengi katika Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita; njaa kuu ikaingia inchi yote: 26 wala hakutumwa Eliya kwa mmojawapo wao, illa kwa mjane mmoja wa Sarepta, mji wa Sidon. 27 Tena palikuwa wengi wenye ukoma katika Israeli zamani za nabii Elisha: wala hapana aliyetakasika illa Naaman, mtu wa Sham. 28 Wakajazwa hasira wote katika sunagogi walipoyasikia haya. 29 Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hatta ukingo wa kilima kile kilichojengwa mji wao, wapate kumporomosha: 30 lakini yeye akapita katikati yao akaenda zake. 31 Akashukia Kapernaum, mji wa Galilaya, akawa akifundisha siku ya sabato: 32 wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa sababu neno lake lilikuwa na uweza. 33 Na palikuwapo katika sunagogi yao mtu mwenye roho ya pepo mchafu: akapaaza sauti kwa nguvu, akinena, 34 Ah, tuna nini nawe Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu. 35 Yesu akamkemea, akinena, Fumba kinywa, mtoke. Yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka, asimdhuru. 36 Ushangao ukawashika wote, wakaambiana wao kwa wao, wakinena, Neno gani hili, maana kwa mamlaka na uweza awaamuru pepo wachafu, nao watoka? 37 Khabari zake zikaenea katika inchi zilizo kando kando killa pahala. 38 Akatoka katika sunagogi, akaingia nyumba ya Simon. Bassi mkwewe Simon alikuwa ameshikwa na homa kali, wakamwomba kwa ajili yake. 39 Akasimama karibu nae akaikemea ile homa, ikamwacha; marra akaondoka akawakhudumu. 40 Hatta jua lilipokuwa likichwa watu wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbali mbali wakawaleta kwake: nae akaweka mikono yake juu ya killa mmoja, akawaponya. 41 Pepo wakawatoka wengi wakipaaza sauti zao wakisema, Wewe u Kristo, Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walijua ya kuwa yeye ndiye Kristo. 42 Hatta ulipokuwa mchana akatoka akaenda mahali pasipokuwa na watu: makutano wakamtafutatafuta, wakamfikilia, wakataka kumzuia asiondoke kwao. 43 Akawaambia, Imenipasa kukhubiri khabari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia: maana kwa hiyo nalitumwa. 44 Akawa akikhubiri katika sunagogi za Galilaya. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania