Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Tiberio Kaisari, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Yahudi, na Herode tetrarka wa Galilaya, na Filipo ndugu yake tetrarka wa Iturea, na wa inchi ya Trakoniti, na Lusania tetrarka wa Abilene,

2 wakati wa ukuhani ukuu wa Anna na Kayafa, neno la Mungu likamfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani.

3 Akalika inchi yote iliyo kando ya Yardani, akikhuhiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi,

4 kaina ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya, Sauti yake apigae mbiu jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake.

5 Killa bonde litajazwa, Na killa jabali na mlima utashushwra, Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na njia zilizoparuza zitakuwa njia sawa;

6 Na wote wenye mwili watanona wokofu wa Mungu.

7 Bassi akawaambia makutano waliotokea illi kubatizwa nae, Enyi uzao wa nyoka, ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu itakayokuja?

8 Zaeni, bassi, matunda yapatanayo na toba wala msianze kusema ndani ya nafsi zenu, Tunae baba ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni, ya kwamba Mungu katika mawe haya aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.

9 Na sasa hivi shoka limekwisha kutiwa katika shina la miti, bassi killa mti usiozaa matunda mema hukatwa ukatupwa motoni.

10 Nao makutano wakamwuliza wakinena, Tufanyeni, bassi?

11 Akajibu akawaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe yeye asiye nayo, na mwenye vyakula, na afanye vivyo hivyo.

12 Watoza ushuru nao wakaja illi kubatizwa, wakamwambia, Mwalimu, tufanyeni?

13 Akawaambia, Msifoze kitu zaidi ya vile mlivyoamriwa.

14 Askari nao wakamwuliza wakisema, Nasi tufanyeni? Akawaambia, Msimtende jeuri mtu aliye yote, wala msitoze kitu bila haki; tena mwe radhi na mshsahara wenu.

15 Bassi wale watu walipokuwa katika hali ya kutazamia, wakitafakari wote khabari za Yohana, kwamba yeye huenda akawa Kristo,

16 Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto:

17 pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; afakusanya nganu yake ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.

18 Bassi kwa maonyo mengi na ya namna nyingine mengi akawakhubiri watu.

19 Lakini Herode tetrarka, akikaripiwa nae kwa ajili ya Herodias, mke wa Filipo, ndugu yake, na kwa ajili ya maovu yote aliyoyafanya Herode,

20 akaongeza na hili jun ya yote, alimfunga Yohana gerezani.

21 Na watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu nae akiisha kubatizwa, na akisali, mbingu zilifunuka.

22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama hua, sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe mwana wangu, mpendwa wangu, ndiwe unipendezae.

23 Nae Yesu mwenyewe alipokuwa akianza kufundisha, umri wake amekuwa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa mwana wa Yusuf, wa Eli,

24 wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yanna, wa Yusuf,

25 wa Matathia, wa Amos, wa Nahum, wa Esli, wa Nagai,

26 wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yosef, wa Yuda,

27 wa Yohana, wa Resa, wa Zorobabel, wa Salathiel, wa Neri,

28 wa Melki, wa Addi, wa Kosan, wa Elmadam, wa Eri,

29 wa Yesua, wa Eliezer, wa Yorim, wa Mathati, wa Lawi,

30 wa Sumeon, wa Yuda, wa Yusuf, wa Yona, wa Eliakim,

31 wa Melea, wa Mainan, wa Mattatha, wa Nathan, wa Daud,

32 wa Yese, wa Obed, wa Boaz, wa Salmon, wa Nahason,

33 wa Aminadab, wa Aram, wa Esrom, wa Fares, wa Yuda,

34 wa Yakob, wa Isaak, wa Ibrahimu, wa Tara, wa Nahor,

35 wa Saruhu, wa Ragau, wa Faleg, wa Eber, wa Sala,

36 wa Kainan, va Arfaksad, wa Sem, wa Nuhu, wa Lamek,

37 wa Methusala, wa Enok, wa Yared, wa Maleleel, wa Kainan,

38 wa Enos, wa Seth, wa Adamu, wa Mungu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo