Luka 24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 HATTA siku ya kwanza ya juma, ikianza kupambazuka, wakaenda kaburini wakiyaleta yale manukato waliyoyaweka tayari, na wengine pamoja nao. 2 Wakalikuta lile jiwe limefingirishwa mbali ya kaburi. 3 Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu. 4 Ikawa wangali wakishangaa kwa haya, kumbe! watu wawili wakisimama karibu yao, wamevaa nguo za kumetameta. 5 Nao wakiingiwa na khofu na kuinama kifudifudi hatta inchi, wakawaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hayi katika wafu? Hayupo hapa, bali amefufuka. 6 Kumbukeni jinsi alivyosema nanyi alipokuwa hajatoka Galilaya, akinena, 7 ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kutiwa katika mikono ya watu wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tafu. 8 Wakakumbuka maneno yake, 9 wakarejea kutoka kaburi, wakawaarifu wale edashara na wale wengine wote pia mambo hayo yote. 10 Na hao waliowaambia mitume mambo haya ni Mariamu Magdalene, na Yoanna, na Mariamu mama yake Yakobo na wengine waliokuwa pamoja nao. 11 Maneno yao yakaonekana kuwa ni upuzi kwao, wala hawakuwasadiki. 12 Lakini Petro akaondoka, akaenda mbio kaburini, akainama, akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vimewekwa peke yake, akarudi kwake, akistaajabu kwa yale yaliyotokea. 13 Siku ileile wawili wao walikuwa wakienda hatta kijiji, jina lake Emmao, kilichokuwa mbali ya Yerusalemi yapata stadio sittini. 14 Nao wakawa wakizumgumza haya yote yaliyotukia. 15 Ikawa katika kuzumgumza kwao na kuulizana, Yesu mwenyewe akakaribia, akafuatana nao. 16 Macho yao yakafumbwa, wasipate kumtambua. 17 Akawaambia, Maneno gani haya mnayobishana katika kutembea kwenu? na tena nyuso zenu zimekunjamana. 18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemi, usiyajue yaliyokuwa ndani yake siku hizi? 19 Akawaambia, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu Mnazareti, aliyekuwa mtu nabii mwenye nguvu kwa tendo na kwa neno mbele za Mungu na watu wote; 20 na jinsi makuhani wakuu na wakubwa wetu walivyomtoa kwa hukumu ya kufa, wakamsulibisha; 21 nasi twalitaraja ya kuwa yeye ndiye atakaekomboa Israeli. Hatta pamoja na haya yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipokuwa haya. 22 Kuna tena wanawake wengine wa kwetu waliotustusha, wakiamkia mapema kwenda kaburini: 23 wasioukuta mwili wake, wakaja, wakasema ya kwamba wametokewa na malaika, waliowaambia yu hayi. 24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi wakaenda kaburini, wakaona vivyo hivyo kama wanawake walivyosema; illa yeye hawakumwona. 25 Nae akawaambia, Enyi wapumbavu, na wenye mioyo mizito katika kuyaamini yote waliyoyasema manabii! 26 Haikumpasa Kristo kupata mateso haya, ndipo aingie enzini mwake? 27 Akaanza toka Musa na manabii, akawafasiria katika maandiko yote mambo yaliyomkhusu yeye. 28 Wakakikaribia kijiji walikokuwa wakienda; nae akajifanya kama anataka kwenda mbele. 29 Wakamshurutisha, wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa maana kumekuchwa, na mchana unakwisha sasa. Akaingia kukaa nao. 30 Ikawa, akiketi pamoja nao, akautwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawagawia. 31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua, akatoweka asionekane nao. 32 Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwa ikiwaka ndani yetu, alipokuwa akisema nasi njiani, akitufunulia maandiko? 33 Wakaondoka saa ileile, wakarudi Yerusalemi, wakawakuta wale edashara wamekusanyika, nao waliokuwa pamoja nao, 34 wakisema, Hakika Bwana amefufuka, amemtokea Simon. 35 Nao wakawahadithia yale ya njiani, na jinsi alivyotambulikana nao kwa kumega mkate. 36 Walipokuwa wakisema hivyo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akiwaambia, Amani kwenu. 37 Wakafadhaika, wakaingiwa na khofu, wakidhani ya kuwa wanaona pepo. 38 Akawaambia, Mbona mmefadhaika? na kwa nini mashaka yanatokea mioyoni mwenu. 39 Tazameni mikono yangu, na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nipapaseni, mkatazame; kwa maana pepo hana mwili na mifupa, kama mnionavyo mimi kuwa nayo. 40 Na baada ya kusema haya akawaonyesha mikono yake na miguu yake. 41 Bassi, wakiwa bado kuamini kwa furaha, wakitaajabu, akawaambia, Mna kitu cha kula hapa? 42 Wakampa kipande cha samaki kilichookwa na asali kidogo. 43 Akakitwaa, akala mbele yao. 44 Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi. 45 Ndipo akaamsha akili zao, wapate kuyatambua maandiko matakatifu. 46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, na ndivyo ilivyompasa Kristo kuteswa, na kufufuka siku ya tatu; 47 na mataifa yote wakhubiriwe kwa jina lake toba na ondoleo la dhambi, kuanzia Yerusalemi. 48 Nanyi mashahidi wa mambo haya. 49 Angalieni, bassi, naituma ahadi ya Baba yangu kwenu: lakini kaeni katika mji huu Yerusalemi, hatta mtakapovikwa nguvu zitokazo juu. 50 Akawaongoza nje mpaka Bethania: akainua mikono yake, akawabariki. 51 Ikawa katika kuwabariki, akajitenga nao, akachukuliwa juu mbinguni. 52 Nao wakamsujudia, wakarudi Yerusalemi na furaha kuu: 53 wakawa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu na kumhimidi. Amin. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania