Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WAKAONDOKA jamii yote, wakamleta kwa Pilato.

2 Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona mtu huyu amipotosha taifa letu, anawakataza watu wasimpe Kaisari kodi, akisema ya kwamba yeye mwenyewe yu Kristo, mfalme.

3 Pilato akamwuliza, akisema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu, akamwambia, Unasema wewe.

4 Pilato akawaambia makuhani wakuu na makutano, Mimi sioni khatiya yo yote katika mtu huyu.

5 Nao wakamshurutisha, wakisema, Awataharakisha watu, akifundisha katika Yahudi yote, akianzia Galilaya hatta hapa.

6 Pilato aliposikia neno hili Galilaya, akauliza, Mtu huyu ni Mgalilaya?

7 Alipojua ni chini ya mamlaka ya Herode, akampeleka kwa Herode; nae alikuwa katika Yerusalemi siku zile.

8 Na Herode alipomwona Yesu, akafurahiwa sana: kwa kuwa tangu zamani alikuwa akitaka kumwona, kwa sababu amesikia mambo yake; akataraja kuona ishara inafanyika nae.

9 Akamwuliza kwa maneno mengi, yeye asimjibu lo lote.

10 Wakasimama makuliani wakuu na waandishi, wakimshitaki kwa nguvu.

11 Bassi Herode akamtweza pamoja na askari zake akamdhihaki, akamvika mavazi mazurimazuri, akamrudisha kwa Pilato.

12 Ndipo Herode na Pilato wakapatana, siku ileile; kwa maana kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao.

13 Pilato akawaita pamoja makuhani wakuu, na wakubwa, na watu, akawaambia,

14 Mmeniletea mtu huyu, kana kwamba anapotosha watu; nami hassi nilipomhukumu mbele yenu, sikuona khatiya katika mtu huyu katika yale mliyomshitaki;

15 wala Herode nae; kwa maana naliwapelekeni kwake, wala hapana neno la kustahili kufa lililotendwa nae.

16 Bassi nikiisha kumrudi, nitamfungua.

17 Maana ilimlazimu kuwafungulia mmoja wakati wa siku kuu.

18 Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mchukue huyu, tufungulie Barabba.

19 Nae ni mtu aliyetiwa gerezani kwa sababu ya fitina iliyofanyika mjini, na kwa uuaji.

20 Bassi marra ya pili Pilato akasema nao, akitaka kumfungua Yesu.

21 Nao wakalia, wakisema, Msulibishe, msulibishe.

22 Nae akawaambia marra ya tatu, Kwani? ubaya gani alioutenda huyu? sikuona hatta neno kwake la kustahili kufa; bassi nikiisha kumrudi nitamfungua.

23 Lakini wakakaza kusema kwa santi kuu, wakitaka asulibiwe; zikashinda sauti zao na za makuhani wakuu.

24 Pilato akakata maneno yafanyike waliyoyataka.

25 Akamfungua yeye aliyetiwa gerezani kwa fitina na uuaji, waliyemtaka: akatoa Yesu kwa mapenzi yao.

26 Walipokuwa wakimchukua, wakamshika Mkurene Simon, aliyekuwa akitoka shamba, wakamtwika yeye msalaba, auchukue nyuma yake Yesu.

27 Wakamfuata makutano mengi ya watu, na ya wanawake, waliojipigapiga, wakaomboleza.

28 Yesu akawageukia, akasema, Binti za Yerusalemi, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.

29 Kwa maana siku zinakuja watakaposema, Wa kheri walio tassa, na matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha.

30 Ndipo watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Tusetirini.

31 Kwa kuwa wakifanya haya wakati wa mti ulio mbichi, wakati wa ule ulio mkavu yatakuwaje?

32 Wakachukuliwa wawili tena, wakhalifu, wauawe pamoja nae.

33 Hatta walipofika pahali paitwapo Kichwa, ndiko walikomsulibisha, na wale wakhalifu, mmoja mkono wa kuume, na mmoja mkono wa kushoto.

34 Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo. Wakagawanya nguo zake, wakipiga kura.

35 Watu wakasimama, wakitazama. Nao wakuu wakamfanyizia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe nafsi yake, kama huyu ndiye Kristo wa Mungu, mtenle wake.

36 Askari wakamdhihaki, wakimjia, wakimpa siki, na kusema,

37 Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, njiokoe nafsi yako.

38 Palikuwa na anwani juu yake kwa harufi za kiyunani na kirumi na kiebrania, HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.

39 Mmoja wa wale wakhalifu waliotundikwa akamtukana, akisema, Si wewe uliye Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.

40 Wa pili akajibu, akamkemea akasema, Humwogopi wewe hatta Mungu, ukiwa katika hukumu ile ile?

41 Na sisi kweli ina haki; kwa maana sisi tunalipwa ijara ya haki ya matendo yetu: bali huyu hakutenda neno lisilofaa.

42 Akamwambia Yesu, Bwana, unikumbuke ujapo katika ufalme wako.

43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo utakuwa pamoja nami Peponi.

44 Ikapata kama saa a sita, pakawa giza juu ya inchi yote hatta saa a tissa,

45 jua likipunguka: pazia ya hekalu ikapasuka katikati.

46 Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu: na alipokwisha kusema haya akatoa roho.

47 Akida alipoona lililokuwa, akamtukuza Mungu, akisema, Kwa kweli mtu huyu alikuwa mwenye haki.

48 Na makutano wote waliokusanyika kutazama haya, walipotazama yaliyofanyika, wakarudi, wakijipiga vifua.

49 Marafiki zake wote wakasimama kwa mbali, nao wanawake waliofuatana nae toka Galilaya, wakiangalia haya,

50 Akatoka mtu, jina lake Yusuf, nae ni mtu wa baraza yao, mtu mwema, mwenye haki

51 (mtu huyu hakuwa akikubali shauri lao wala tendo lao), mwenyeji wa Arimathaya, mji wa Wayahudi, nae mwenyewe akiutazamia ufalme wa Mungu.

52 Bassi mtu huyu akamwendea Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu.

53 Akaushusha, akauzinga nguo za katani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani; hajawekwa mtu aliye yote ndani yake kamwe.

54 Ilikuwa siku ya Maandalio, sabato ikawadia.

55 Wanawake wakafuatana nao, wale waliokuja pamoja nae kutoka Galilaya, wakalitazama kaburi na jinsi ulivyowekwa mwili wake. Wakarudi wakafanya tayari manukato na marhamu.

56 Na siku ya sabato wakastarehe kama ilivyoamriwa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo