Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKAINUA macho yake akawaona watu wakitia sadaka zao katika sanduku ya hazina, watu matajiri.

2 Akamwona na mjane mmoja maskini, akitia robo pesa mbili.

3 Akasema, Amin, nawaambieni, Huyu mjane maskini ametia vingi kuliko wote:

4 kwa maana hawa wote wametia katika sadaka za Mungu baadhi ya mali iliyowazidi, bali huyu katika mahitaji yake ametia vitu vyote alivyokuwa navyo.

5 Hatta watu kadha wa kadha walipokuwa wakinena khabari za hekalu, ya kama lilipambwa kwa mawe mazuri, na sadaka za watu, akasema,

6 Haya mnayoyatazama, siku zitakuja, halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.

7 Wakuimwuliza, wakisema, Mwalimu, haya yatakuwa lini, bassi? Na nini dalili ya kuwa haya yote ni karibu ya kutimia?

8 Akasema, Jibadharini, msidanganyike; kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ndiye, na, Majira yamekaribia. Bassi, msiwafuate hawo.

9 Nanyi mtakaposikia khabari za vita na fitina msitishwe: maana haya hayana buddi kutukia kwanza, lakini mwisho wenyewe hauji marra moja.

10 Kiisha akawaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme:

11 kutakuwa na matetemeko makubwa ya inchi mahali mahali, na njaa, na tauni. Kutakuwa na mambo ya kutisha, na ishara kuu kutoka mbinguni.

12 Lakini kabla ya haya yote watawakamateni na kuwaudhini, watawapelekeni mbele ya sunagogi na gerezani, mkichukuliwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu.

13 Lakini haya yatapata kuwa ushuhuda wenu.

14 Azimuni bassi mioyoni mwenu, msitafakari mbele mtakavyojibu.

15 Kwa maana mimi nitawapeni kinywa na hekima, ambayo watesi wenu hawataweza kuikana wala kushindana nayo.

16 Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha wengine wenu.

17 Mtachukizwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.

18 Na unywele wa vichwa vyenu hautapotea kamwe.

19 Kwa subira yenu mtazipata robo zenu.

20 Lakini, mtakapoona Yerusalemi unazungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kuwa uharibifu wake umekaribia.

21 Ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani, na walio katikati yake watoke waende zao, na walio shambani wasiuingie.

22 Kwa sababu hizi ni siku ya mapatilizo, yote yaliyoandikwa yapate kutimizwa.

23 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku zile! kwa maana itakuwa shidda kuu juu ya inchi, na ghadhabu juu ya watu hawa.

24 Nao wataanguka kwa ukali wa upanga, watachukuliwa mateka mpaka mataifa yote: nao Yerusalemi utakanyagwa na mataifa, hatta majira ya mataifa yatakapotimia.

25 Na kutakuwa ishara katika jua na mwezi na nyota: na katika inchi dhiiki ya mataifa, wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake;

26 watu wakizimia kwa khofu, na kwa kutazamia yanayoujia ulimwengu; kwa maana nguvu za mbingu zitatikisika.

27 Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu kwa nguvu na utukufu mwingi.

28 Bassi hayo yaanzapo kuwa, tazameni juu, mkainue vichwa vyenu kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.

29 Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti yote;

30 iishapo kuchupua, mwaona na kutambua nafsini mwenu ya kwamba mavuno yameisha kuwa karibu.

31 Nanyi vivyo hivyo mwonapo hayo yanakuwa, tambueni ya kuwa ufalme wa Mungu u karibu.

32 Amin, nawaanibieni, Kizazi hiki hakitapita kamwe hatta haya yote yatimizwe.

33 Mbingu na inchi zitapita; bali maneno yangu hayatapita kamwe.

34 Bassi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi, na masumbufu ya maisha haya,

35 siku ile ikawajieni kwa ghafula, kama mtego, maana hivyo ndivyo itakavyowajia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia yote.

36 Kwa hiyo kesheni killa wakati, mkiomba mpate kuhesabiwa kuwa mmestahili kuponea haya yote yatakayokuwa, na kusimama mahali penu mbele ya Mwana wa Adamu.

37 Bassi killa siku alikuwa akifundisha hekaluni wakati wa mchana; na wakati wa usiku akitoka, na kulala katika mlima uitwao mlima wa mizeituni.

38 Watu wote wakaamka mapema wakamwendea alfajiri mle hekaluni illi kumsikiliza.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo