Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA siku zile kulitoka amri kwa Kaisari Augusto ya kama iandikwe orodha ya majina ya walimwengu wote:

2 orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa wakati Kurenio alipotawala Sham.

3 Watu wote wakashika njia kwenda kuandikwa, killa mtu mjini kwake.

4 Na Yusuf nae akaondoka Galilaya kutoka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Yahudi hatta mji wa Daud, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye wa nyumba na jamaa ya Daud,

5 illi aandikwe pamoja na Mariamu mkewe ambae ameposwa nae; nae ana mimba.

6 Ikawa katika kukaa kwao huko, siku zake za kuzaa zikatimia.

7 Akamzaa mtoto wake wa kifungua mimba, akamfunga nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakuona nafasi katika nyumba ya wageni.

8 Katika inchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni usiku na kulinda kundi lao kwa zamu.

9 Malaika wa Bwana akawatokea, utukufu wa Bwana ukawangʼaria: wakaingiwa na khohi nyingi.

10 Malaika akawaambia, Msifanye khofu; kwa maana nawaletea ninyi khabari njema za furaha kuu, itakayokuwa kwa watu wote:

11 maana leo katika mji wa Daud amezaiiwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana.

12 Na hii ni ishara kwenu: Mtamkuta mtoto amefungwa nguo za kitoto; amelazwa horini.

13 Ghafula hiyo walikuwapo pamoja na yule malaika wengi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, wakisema,

14 Utukufu una Mungu palipo juu, Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia.

15 Ikawa malaika walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakaambiana, Haya na twende zetu mpaka Bethlehemu, tukaone neno hili lililofanyika, Bwana alilotujulisha.

16 Wakaenda kwa haraka, wakamkuta Mariamu na Yusuf, na mtoto amelazwa horini.

17 Walipoona wakaeneza khabari za neno waliloambiwa, la huyu mtoto.

18 Wote waliosikia wakataajabu kwa yale waliyoambiwa na wachungaji.

19 Bali Mariamu aliyahifadhi maneno haya yote akiyatafakari moyoni.

20 Wachungaji wakarudi, wakimtukuza Mungu na kumhimidi kwa mambo yote waliyosikia, na waliyoona, kwa namna waliyoambiwa.

21 Na zilipotimia siku nane za kumtahiri, alikwitwa jina lake Yesu, lile lililotajwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.

22 Nazo siku za kutakasika kwao zilipotimia, kwa sharia ya Musa, wakamleta Yerusalemi, wampe Bwana;

23 (kama ilivyoandikwa katika sharia ya Bwana, Killa mume afunguae tumbo la mama yake aitwe mtakatifu kwa Bwana;)

24 wakatoe sadaka kama ilivyonenwa katika sharia ya Bwana, Hua wawili, au makinda ya njiwa mawili.

25 Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae.

26 Nae alikuwa amebashiriwa na Roho Mtakatifu ya kwamba haoni mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

27 Bassi akaja hekaluni kwa roho: na wazee wake walipomleta mtoto Yesu, wamfanyie kwa desturi ya sharia,

28 mwenyewe akampokea mikononi mwake, akimhimidi Mungu, akasema,

29 Sasa wamrukhusu, Bwana, mtumishi wako kwa amani, Kama ulivyosema:

30 Kwa kuwa macho yangu yamenona wokofu wako,

31 Uuliouweka tayari machoni pa watu wote;

32 Nuru ya kuwaangaza mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.

33 Yusuf na mama yake wakawa wakistaajahu kwa yale yaliyonenwa juu yake;

34 Sumeon akawabariki, akamwambia Mariamu, mama yake, Hakika huyu amewekwa, waanguke, wasimame wengi katika Israeli; awe ishara inenwayo;

35 hatta na wewe upanga utakupenya roho yako; illi yafumike mawazo ya mioyo mingi.

36 Kulikuwa na Auna, nabii mke, binti Fanueli, wa kabila ya Asher; nae kongwe wa siku nyingi, amekuwa na mume miaka saba baada ya ujana wake;

37 nae mjane wa miaka themanini na mine; asiyeondoka hekaluni, kwa kufunga na kusali akiabudu usiku na mchana.

38 Akitokea yeye nae saa ileile, alimshukuru Mungu, akawapasha khabari zake watu wote waliokuwa wakitazamia ukombozi katika Yerusalemi.

39 Nao walipokwisha kuyatimiza yote yaliyomo katika sharia ya Bwana, wakarudi Galilaya hatta mji wao Nazareti,

40 Mtoto yule akakua, akaongezeka nguvu, akajazwa hekima; neema ya Mungu ikawa pamoja nae.

41 Bassi wazee wake, killa mwaka walikuwa wakienda Yerusalemi siku kuu ya Pasaka.

42 Hatta alipopata miaka kumi na miwili, wakapanda kwenda Yerusalemi, kama ilivyokuwa desturi ya siku kuu:

43 na wakiisha kuzitimiza siku, walipokuwa wanarudi kwao, yule mtoto Yesu akabaki nyuma Yerusalemi, wala mama yake na Yusuf hawakujua;

44 wakadhani yumo katika msafara yao, wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao,

45 wasimwone, wakarejea Yerusalemi, wakimtafuta.

46 Ikawa baada ya siku tatu, wakamwona hekaluni, ameketi kati ya waalimu, akiwasikiliza, na kuwauliza.

47 Wote waliomsikia wakataajahu kwa akili zake na majibu yake.

48 Nao walipomwona wakashangaa sana; mama yake akamwambia, Mwanangu, kwani ukatutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.

49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwa katika nyumba ya baba yangu?

50 Wala hawakuelewa na neno lile alilowaanibia.

51 Akashuka pamoja nao, akafika Nazareti, akawa anawatii: mama yake akayahifadhi maneno haya yote moyoni mwake.

52 Yesu akazidi kuendelea katika hekima, na kimo, na neema kwa Mungu na kwa watu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo