Luka 19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 AKAINGIA Yeriko akawa akipita katikati yake. 2 Na tazama, mtu mmoja, jina lake alikwitwa Zakkayo, mkubwa wa watoza ushuru, nae tajiri: 3 akatafuta kumwona Yesu, ni mtu gani, asiweze lakini kwa sababu ya makutano, maana kimo chake alikuwa mfupi. 4 Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa sababu alitaka kupita njia ile. 5 Na Yesu, alipofika mahali pale, akatazama juu, akamwona, akamwambia, Zakkayo, shuka upesi; maana leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. 6 Akashuka upesi, akamkaribisha kwa furaha. 7 Hatta watu walipoona wakanungʼunika wote, wakisema, ya kama, Ameingia akae kwa mtu mwenye dhambi. 8 Zakkayo akasimama, akamwambia Bwana, Bwana, nussu ya mali zangu ninawapa maskini; na kama nimetoza mtu kitu kwa kumsingizia uwongo ninamrudishia marra nne. 9 Yesu akamwambia, Leo wokofu umefika nyumbani humu, kwa kuwa huyu nae ni mwana wa Ibrahimu. 10 Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja illi kutafuta kilichopotea na kukiokoa. 11 Nao wakisikia haya akaongeza akawaambia mfano, kwa sababu alikuwa akikaribia Yerusalemi, nao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana marra moja. 12 Bassi akasema, Mtu mmoja, mungwana, alisafiri kwenda inchi ya mbali illi kujipatia ufalme na kurejea. 13 Akawaita watu kumi katika watumishi wake, akawapa mane za fedha kumi, akawaambia, Fanyeni biashara hatta nitakaporudi. 14 Wenyeji wake wakanichukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatutaki mtu huyu atutawale. 15 Ikawa aliporejea, baada ya kuupokea ufalme, akatoa amri waitwe wale watumishi aliowapa ile fedha, apate kujua jinsi walivyofanya biashara. 16 Wa kwanza akaja akasema, Bwana, mane yako imepata mane kumi. 17 Akasema, Vema, mtumishi mwema, kwa sababu umekuwa mwaminifu kwa kitu kilicho kidogo, bassi, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. 18 Akaja wa pili, akisema, Mane yako, Bwana, imepata mane tano. 19 Akamwambia yule nae, Na wewe uwe juu ya miji mitano. 20 Akaja mwingine akasema, Bwana, tazama, mane yako hii niliyokuwa nayo, imewekwa akiba katika leso: 21 maana nalikuogopa, kwa sababu wewe mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. 22 Akamwambia, Kwa kinywa chako nitakuhukumu, ee mtumishi mwovu wewe. Ulijua ya kuwa mimi mtu mgumu, naondoa nisichoweka, navuna nisichopanda; 23 mbona, bassi, hukuweka fedha yangu kwao watoao riba, nami nikija ningaliipata pamoja na faida? 24 Akawaambia waliohudhuria, Mnyangʼanyeni mane yake moja mkampe yule mwenye mane kumi. 25 (Wakamwambia, Bwana, ana mane kumi). 26 Maana nawaambieni, Killa aliye na kitu, atapewa, bali yeye asiye na kitu hatta kile alicho nacho atanyangʼanywa. 27 Walakini wale adui zangu wasiotaka niwatawale, waleteni huku mkawachinje mhele zangu. 28 Alipokwisha kusema haya, akaendelea mbele, akipanda kwenda Yerusalemi. 29 Hatta alipokaribia Bethfage na Bethania karibu ya mlima wa mizeituni, akatuma wawili katika wanafunzi wake, akisema, 30 Enendeni zenu hatta kile kijiji kinachowakabili ninyi, na mkiingia ndani, mtaona mwana punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni. 31 Na mtu akiwaambieni, Mbona mnamfungua? semeni hivi, Bwana ana haja nae. 32 Bassi, wale waliotumwa wakaenda, wakaona vile vile kama alivyowaambia. 33 Na walipokuwa wakimfungua mwana punda, wenyewe wakawauliza, Mnamfunguliani huyu mwana punda? 34 Wakasema, Bwana ana haja nae. 35 Wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao juu ya yule mwana punda wakampandisha Yesu. 36 Nae alipokuwa akienda, wakatandaza nguo zao njiani. 37 Hatta alipokuwa amekwisha kukaribia matelemko va mlima wa mizeituni, kundi lote la wanafunzi wake wakaanza kufurahi na kumhimidi Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya miujiza yote waliyoiona, 38 wakinena Amebarikiwa mfalme ajae kwa jina la Bwana, amani mbinguni, na utukufu palipo juu. 39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, wakemee wanafunzi wako. 40 Akajibu, akasema, Nawaambieni kwamba, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele. 41 Nae alipokaribia akauona mji, akaulilia, 42 akasema, Laiti ungalijua siku hii yaliyo ya amani! lakini sasa yamefichwa machoni mwenu; 43 Kwa maana siku zitakujilia, adui zako watakapokujengea boma; watakuzunguka, watakudhiikisha pande zote; 44 watakuangusha chini, na watoto wako ndani yako; wasikuachie jiwe juu ya jiwe; kwa kuwa hukujua majira ya kujiliwa kwako. 45 Akaingia hekaluni, akaanza kuwatoa wakuzao na wanunuao ndani yake; akiwaambia, 46 Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi. 47 Akawa akifundisha killa siku hekaluni, makuhani wakuu na waandishi na wakubwa wa watu wakatafuta kumwangamiza, 48 nao bawakuona la kutenda; maana watu wote waliambatana nae, wakimsikiliza. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania