Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKAWAAMBIA na mfano ya kama imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa,

2 akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani; hamchi Mungu wala hajali mtu.

3 Na katika mji huo palikuwa na mjane aiiyemwendeaendea, akisema, Nipatie haki yangu, ukaniokoe na adui yangu.

4 Nae hakukubali muda wa siku kadha wa kadha; khalafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa mimi simchi Mungu wala sijali mtu;

5 illakini kwa kuwa mjane huyu ameniudhi, nitampatia haki yake, asije akanidhoofisha kwa kunijia daima.

6 Bwana akasema, Sikieni asemavyo yule kadhi asiye haki.

7 Bassi Mungu je! hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, nae ni mvumilivu kwao? Nawaambieni atawapatia haki upesi.

8 Walakini Mwana wa Adamu atakapokuja, je! ataiona imani duniani?

9 Yesu akawaambia mfano huu watu waliojidhani nafsi zao kuwa wenye haki, wakiwadharau wengine wote.

10 Watu wawili walipanda hekaluni kusali; mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.

11 Yule Farisayo akasimama, akasali hivi kwa nafsi yake, Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine, wanyangʼanyi, wazinzi, waia kama na huyu mtoza ushuru.

12 Nafunga marra mbili kwa juma; nalipa zaka za mapato yangu yote.

13 Na yule mtoza ushuru akasimama mbali, asitake hatta kuinua macho yake mbinguni; hali akajipigapiga kifua, akisema, Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.

14 Nawaambia ninyi, huyu alishuka nyumbani kwake amepata kibali kuliko yule: kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.

15 Bassi wakamletea hatta watoto wachanga illi awaguse; lakini wanafunzi wake walipoona wakawakaripia.

16 Bali Yesu akawaita waje kwake, akisema, Waacheni watoto waje kwangu, kwa maana watu kama hawo ufalme wa Mungu ni wao.

17 Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto, hatauingia kamwe.

18 Na mtu mkuhwa mmoja akamwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele?

19 Yesu akamwambia, Mbona waniita mwema? Hakuna mwema illa mmoja ndiye Mungu.

20 Wazijua amri, Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudu uwongo, Waheshimu baba yako na mama yako.

21 Akasema, Haya yote nimeyashika tangu ujana wangu.

22 Yesu aliposikia haya, akamwambia, Neno moja hujalipata bado; viuze vitu vyote ulivyo navyo, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kiisha, njoo unifuate.

23 Lakini aliposikia maneno haya akafanya huzuni nyingi: maana alikuwa mtu tajiri sana.

24 Bassi Yesu alipoona ya kuwa amefanya huzuni nyingi, akasema, Kwa shidda gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu.

25 Kwa maana ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

26 Nao waliposikia, wakasema, Nani, bassi, awezae kuokoka?

27 Akasema, Yasiyowezekana kwa wana Adamu, yawezekana kwa Mungu.

28 Petro akasema, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe.

29 Akawaambia, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au wazazi, au ndugu, au mke, au watoto kwa ajili ya ufalme wa Mungu,

30 illa atapokea zaidi marra nyingi sasa wakati huu, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.

31 Bassi, Yesu akawachukua wale thenashara akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemi, na yatatimizwa mambo yote aliyoandikiwa Mwana wa Adamu na manabii.

32 Kwa maana atatiwa katika mikono ya Mataifa, atafanyiwa dhihaka na kutendwa jeuri, na kutemewa mate;

33 na wakiisha kumpiga mijeledi, watamwua; na siku ya tatu atafufuka.

34 Nao hawakufahamu haya hatta kidogo, neno hili likawa limefichwa kwao, wala hawakuyajua yaliyonenwa.

35 Ikawa alipokaribia Yeriko, pafikuwa na kipofu, amekaa kando ya njia akiomba.

36 Aliposikia makutano yanapita, akauliza khabari, Kuna nini?

37 Wakamweleza, Yesu wa Nazareti anapita.

38 Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daud, unirehemu.

39 Bassi, waliotangulia wakamkemea, anyamaze; lakini yeye akazidi sana kupiga makelele, Mwana wa Daud, unirehemu.

40 Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake;

41 na alipomkaribia akamwuliza, Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwami, nipate kuona.

42 Yesu akamwambia, Upewe kuona imani yako imekuponya.

43 Marra akapata kuona, akamfuata, akimtukuza Mungu; na watu wote walipoona wakampa Mungu sifa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo