Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKAWAAMBIA wanafunzi wake, Mambo ya kukosesha hayana buddi kutokea, lakini ole wake mtu yule ayaletae!

2 Ingemfaa huyu zaidi jiwe la kusagia litiwe shingoni pake akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa hawa wadogo.

3 Jihadharini: ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu, msamehe,

4 na akikosa marra saba katika siku moja, akakurudia marra saba, akisema, Natubu, msamehe.

5 Mitume wakamwambia, Bwana, utuongezee imani yetu.

6 Bwana akasema, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali, mngeuambia mzambarau huu, Ngʼoka ukapandwe baharini, nao ungewatiini.

7 Lakini nani kwenu mwenye mtumishi anaelima, an anaeehunga kondoo? je! amwambia marra atakapoingia, akitoka mashamba, Njoo upesi, keti, ule chakula?

8 La! kinyume cha hayo, atamwambia, Pakua chakula, nile; jifunge, unikhudumie hatta nikiisha kula na kunywa; na baada ya haya utakula na kunywa mwenyewe.

9 Je! amshukuru yule mtumishi kwa sahahu alifanya alivyoamriwa? Sidhani.

10 Kadhalika na ninyi, mkiisha kufanya vyote mlivyoamriwa, semeni, Sisi watumishi wasiofaa; tumetenda yaliyotupasa kutenda.

11 Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemi, alikuwa akipita kati ya Samaria na Galilaya.

12 Alipokuwa akiingia kijiji kimoja, wakakutana nae watu kumi wenye ukoma, waliosimama mbali;

13 nao wakapaaza sauti zao wakisema, Yesu, Bwana, uturehemu.

14 Alipowaona, akawaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa katika kwenda kwao wakatakasika.

15 Mmoja wao akiona ya kuwa amepona, akarudi akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;

16 akaanguka kufudifudi miguuni pake, akimshukuru; nae ni Msamaria.

17 Yesu akajiliu, akasema, Si wote kumi waliotakasika? Wale tissa wa wapi?

18 Hiawakupatikana waliorudi kumpa Mungu sifa zake, illa mgeni huyu.

19 Akamwambia, Simama; enenda zako; imani yako imekuokoa.

20 Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu waja lini? akawajibu, akasema, Ufalme wa Mungu hauji kwa kupelelezwa.

21 Wala hawatasema, Tazama, huko au huko! maana fahamuni! ufalme wa Mungu umo ndani yenu.

22 Akawaambia wanafunzi wake, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku mojawapo ya siku za Mwana wa Adamu wala hamtaiona.

23 Na watawaambieni, Tazama huko, au tazama huko! Msiondoke hapo mlipo wala msiwafuate.

24 Kwa maana kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hatta upande huu chini ya mbingu, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa katika siku yake.

25 Lakini kwanza hana buddi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi biki.

26 Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa na katika siku za Mwana wa Adamu.

27 Walikuwa wakila, wakinywa, wakioa, wakiozwa, hatta siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, gbarika ikafika, ikawaangamiza wote.

28 Vivyo hivyo kama ilivyokuwa siku za Lut: walikuwa wakila, wakinywa, wakimmua, wakiuza, wakipanda, wakijenga;

29 hatta siku ile amhayo Lut alitoka Sodom, kukanya moto na kiberiti kutoka mbinguni, vikawaangamiza wote.

30 Kadhalika itakuwa katika siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.

31 Katika siku ile, aliye juu darini, na vyombo vyake ndani ya nyumba, asishuke illi kuvitwaa: nae aliomo shambani vivyo hivyo asirejee nyuma.

32 Mkumbukeni mkewe Lut.

33 Mtu ye yote atakaeisalimisha roho yake ataiangamiza, na mtu ye yote atakaeitoa ataihifadhi.

34 Nawaambieni, Usiku ule watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja, mmoja atatwaliwa, na mmoja ataachwa.

35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja, mmoja atatwaliwa, na mmoja ataachwa.

36 Watu wawili watakuwa mashambani; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.

37 Wakajibu wakamwambia, Wapi, Bwana? Akawaambia, Mzoga uliko ndiko watakakokutana tai.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo