Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 TENA Yesu akawaambia wanafunzi wake, Kulikuwa na mtu tajiri, aliyekuwa na wakili; huyu akashitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake.

2 Akamwita, akamwambia, Nini hii nisikiayo juu yako? Toa khabari ya uwakili wako, maana huwezi tena kuwa wakili.

3 Yule wakili akasema moyoni, Nifanyeje, kwa maana bwana wangu ananiondolea nwakili? Kulima siwezi; kuomba natahayari.

4 Nimekwisha kujua nitakalotenda, illi, nitolewapo katika nwakili, wanikaribishe nyumbani mwao.

5 Bassi akawaita wadeni wa bwana wake killa mmoja, akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu?

6 Akasema, Tanaki mia za mafuta. Akamwambia, Twaa khati yako; haya, kaa kitako, andika khamsini.

7 Akiisha, akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Mikanda mia ya nganu. Akamwambia, Twaa khati yako, andika themanini.

8 Yule bwana akamsifu wakili asiye haki, kwa kuwa alitenda kwa busara: kwa maana wana wa zamani hizi wana busara kuliko wana wa nuru, katika kizazi chao wenyewe.

9 Na mimi nawaambia ninyi, Jifanyieni rafiki kwa mamona ya udhalimu, illi itakapopunguka wawakaribishe ninyi katika makao ya milele.

10 Aliye mwaminifu katika kile kilicho kidogo huwa mwaminifu na katika kile kilicho kikubwa: nae aliye mdhalimu katika kile kilicho kidogo, huwa mdhalimu na katika kile kilicho kikubwa.

11 Bassi, ikiwa hamkuwa waaminifu katika mamona ya udhalimu, nani atakaewaaminisheni mali ya kweli?

12 Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, nani atakaewapeni mali iliyo yenu wenyewe?

13 Hakuna mtumishi awezae kuwatumikia bwana wawili: maana au atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na Mamona.

14 Mafarisayo nao wakayasikia haya yote, nao walikuwa wakipenda fedha; wakamdhihaki.

15 Akawaambia, Ninyi ndio watu wanaodai kuwa wenye haki mbele ya wana Adamu, lakini Mungu anajua mioyo yenu; kwa maana lililotukuka kwa wana Adamu, ni chukizo mbele ya Mungu.

16 Torati na manabii zilikuwako mpaka Yohana. Tangu wakati ule, khabari njema ya ufalme wa Mungu inakhubiriwa, na killa mtu anauingia kwa nguvu.

17 Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na inchi vitoweke kuliko nukta moja ya torati itanguke.

18 Killa amwachae mkewe na kumwoa mwingine, amezini; nae amwoae yeye aliyeachwa na mumewe azini.

19 Palikuwa na mtu tajiri, aliyevaa porfuro na bafuta, akafanya furaha kilia siku na anasa.

20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, hutupwa mlangoni pake, ana vidonda,

21 akitamani kushibishwa na makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri: hatta mbwa nao huja, humramba vidonda vyake.

22 Ikawa maskini akafa, akachukuliwa na malaika kifuani kwa Ibrahimu. Akafa na yule tajiri, akazikwa.

23 Bassi katika akhera akainua macho yake, akiwa katika adhabu, akamwona Ibrahimu yuko mbali, na Lazaro kifuani pake.

24 Akalia, akasema, Baba Ibrahimu, unirehemu, umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa maana naumia katika moto huu.

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kuwa ulipokea mema yako katika maisha yako, na Lazaro kadhalika mabaya; lakini sasa yeye yupo hapa anafarajiwa, nawe unanmizwa.

26 Na zaidi ya haya yote, kati yetu sisi na ninyi lipo shimo kuhwa limewekwa, hatta watu watakao kutoka huku wasiweze kuja kwenu, wala wale wa huko wasivuke kuja kwetu.

27 Akasema, Bassi, nakuomba, Baha, umtume nyumnani kwa haha yangu;

28 maana nina ndugu watano; awashuhudie, wasije nao mahali hapa pa adhabu.

29 Ibrahimu akasema, Wana Musa na manabii; wawasikilize wao.

30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini akienda kwao mmoja kutoka wafu watatubu.

31 Akamwambia, Wasiposikia Musa na manabii, ajapoondoka mtu katika wafu, hawatashawishwa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo