Luka 14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 IKAWA, Yesu alipoingia katika nyumba ya mtu mmoja, mtu mkuu katika Mafarisayo, siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia. 2 Bassi mbele yake palikuwa mtu hawezi safura. 3 Yesu akajibu akawaambia wana sharia na Mafarisayo, akisema, Je? ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo? Wakanyamaza. 4 Akamtwaa, akamponya, akamrukhusu. 5 Akajibu akawaambia, Nani wenu mwenye punda au ngʼombe ametumbukia kisimani, asiyemwondoa marra moja siku ya sabato? 6 Nao hawakuweza kumjibu kwa haya. 7 Akawaambia mfano wale waliokwitwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya kwanza; akiwaambia, 8 Ukiitwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha kwanza, isiwe labda mwenye sifa kupita zako amekwitwa nae, 9 akaja mwenye kuwaiteni wewe nae, akakuambia, Mpishe huyu; ndipo utaanza kwa aibu kutwaa pahali pa chini. 10 Walakini ukiitwa, enenda ukaketi pahali pa chini: illi akija yeye aliyekuita akuamhie, Rafiki yangu, jongea huku mbele; ndipo utakapokuwa na heshima machoni pao wote waketio pamoja nawe. 11 Kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa. 12 Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha assubuhi au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako walio na mali, wasije na wao wakakualika wewe, ukapata malipo. 13 Bali ufanyapo karamu, wakaribishe maskini, vilema, viwete, vipofu: nawe utakuwa kheri: 14 kwa sababu hawana kitu cha kukulipa; maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki. 15 Bassi mtu mmoja katika hawo walioketi pamoja nae, alipoyasikia haya, akamwambia, Yu kheri atakaekula mkate katika ufalme wa Mungu. 16 Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika watu wengi, 17 akamtuma mtumishi wake saa ya karamu kwenda kuwaambia walioalikwa, Njoni, maana vitu vyote vimekwisha kuwa tayari. 18 Wakaanza kutoa udhuru, wote pia kwa nia moja. Wa kwanza akamwambia, Nimenunua shamba, sina buddi kwenda na kulitazama; nakuomba, unisamehe. 19 Mwingine akasema, Nimenunua ngʼombe, jozi tano: naenda niwajaribu; nakuomba unisamehe. 20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hii siwezi kuja. 21 Yule mtumishi akaenda, akamwarifu Bwana wake mambo haya. Ndipo yule mwenye nyumba akaghadhabika, akamwambia mtumishi wake, Toka upesi ukaende njia kuu na vichochoro vya mji, ukalete hapa maskini, na vilema, na viwete, na vipofu. 22 Yule mtumishi akasema, Yamekwisha kutendeka hayo uliyoniagiza na ingaliko nafasi. 23 Yule Bwana akamwambia mtumishi wake, Kaenda barabarani na mipakani, ukawashurutishe waingie illi nyumba yangu ipate kujaa. 24 Maana nawaambieni ya kwamba katika watu wale walioalikwa hapana hatta mmoja atakaeionja karamu yangu. 25 Bassi makutano mengi wakafuatana nae; akageuka akawaambia, 26 Mtu akija kwangu, nae hamehukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wanaume na wanawake, na uzima wake pia, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 27 Na mfu ye yote asiyechukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuihesabu gharama kama ana vitu vya kuumaliza? 29 Asije akawa hawezi kuumaliza baada ya kuweka msingi, watu wote wakaanza kumdhihaki, wakisema, 30 Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. 31 Au mfalme gani, kama anakwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana nae anaemjia pamoja na watu elfu ishirini? 32 Kama sivyo, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, yule mtu akiwa angali mbali. 33 Bassi, kadhalika killa mmoja wenu asiyeviacha vitu vyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 34 Chumvi ni njema, illakini ile chumvi ikiwa imeharibika, itatiwa nini ikolee? 35 Haiifai inchi wala jaa; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania