Luka 13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 WAKATI huohuo walikuwapo watu wakimwarifu khabari za Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao. 2 Akajibu, akawaambia, Je! Mwadhani ya kuwa Wagalilaya hawo walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote hatta wakapata mateso kama hayo? 3 Nawaambieni sivyo: lakini msipotuhu nyote mtaangamia vivyo hivyo. 4 Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara katika Siloam, ukawaangamiza, mwadhani ya kuwa walikuwa wakosaji kuliko watu wote wakaao Yerusalemi? 5 Nawaanibieni, Sivyo: lakini msipotubu, nyote mtaangamia vivyo hivyo. 6 Akanena mfano huu: Mtu mmoja alikuwa na mtini, umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake wala hakupata. 7 Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda katika mtini huu, nisipate. Ukate, kwa nini uiharibu inchi pia? 8 Akamjibu, akamwambia, Bwana, uache mwaka huu nao, hatta nikaupalilie, na kuusamadi: 9 nao ukizaa matunda, vyema, la! haukuzaa, ndipo utaukata. 10 Akawa akifundisha katika sunagogi mojawapo siku ya sabato. 11 Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu miaka kumi na minane: nae amepindana, asiweze kujiinua kabisa. 12 Bassi Yesu alipomwona, akamwita, akamwambia, Ee mwanamke, umefunguliwa udhaifu wako. 13 Akaweka mikono yake juu yake, akanyoka marra hiyo, akaanza kumtukuza Mungu. 14 Mkuu wa ile sunagogi akajibu, akiona hasira kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akawaambia makutano, Kuna siku sita itupasapo kufauya kazi: katika hizo, bassi, njoni mponywe wala si katika siku ya sabato. 15 Bassi Bwana akamjibu, akasema, Ewe mnafiki, killa mmoja wenu je! hamfungui ngʼombe wake au punda wake mazizini siku ya sabato, akaenda nae kumnywesha? 16 Na huyu, aliye binti Ibrahimu, amhae Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? 17 Na aliposema haya, watu wote walioshindana nae wakatahayarika, mkutano wote wakafurahi kwa ajili ya mambo matukufu yaliyotendwa nae. 18 Bassi, akasema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Na niufananishe na nini? 19 Umefanana na punje ya kharadali, aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake, ikakua, ikawa mti mkubwa, ndege za anga wakatua katika matawi yake. 20 Akasema marra ya pili, Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? 21 Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia. 22 Akawa akizungukazunguka katika miji ni vijiji, akifundisha, na kufanya safari kwenda Yerusalemi. 23 Mtu mmoja akamwambia, Bwana, wao wanaookolewa ni wachaehe? 24 Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba; kwa maana nawaambieni ya kwamba watu wengi watatafuta kuingia nao bawataweza. 25 Tokea wakati ule atakapoondoka mwenye nyumba na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkinena, Bwana, Bwana! utufungulie; nae akajibu, akawaambieni, Siwajui mtokako; 26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula, na kunywa mbele yako; nawe ulifundisha kalika njia zetu; 27 nae atasema, Nawaambieni, Siwajui mtokako: ondokeni mbali nami, ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. 28 Hapo kutakuwako kulia na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaak na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, na ninyi wenyewe nikitupwa nje. 29 Na watakuja watu toka maawio ya jua na machweo yake na toka kaskazini na kusini, nao wataketi katika ufalme wa Mungu. 30 Kafahamuni, wako wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wako wa kwanza watakaokuwa wa mwisho. 31 Siku ile ile baadhi ya Mafarisayo wakamwendea, wakamwambia, Ondoka hapa, ukaende zako: kwa maana Herode anataka kukuua. 32 Akawaambia, Enendeni zenu, nikamwambie yule mbweha, Tazama, nafukuza pepo, nafanya kazi ya kuwaponya watu leo na kesho, nami siku ya tatu nakamilika. 33 Illakini imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa, kwa maana haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemi. 34 Ee Yerusalemi, Yerusalemi, uwauae manabii na kuwapiga mawe wao waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hanikutaka! 35 Angalieni, nyumba yenu imeachwa ukiwa. Amin, nawaambieni, Hamtaniona kabisa hatta wakati ule mtakaposema, Amebarikiwa yeye ajae kwa jina la Bwana. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania