Luka 12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 HUKO nyuma mkutano wa watu, watu elfu nyingi walipokusanyika hatta wakakanyagana, akaanza kuwaambia wanafunzi wake khassa, Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki. 2 Lakini hakuna neno lililofunikwa ambalo halitafunuliwa khalafu, wala lililostirika ambalo halitajulika khalafu. 3 Bassi yo yote mliyoyasema gizani, yatasikiwa katika nuru: nalo mlilolisema katika sikio la mtu katika vyumba vya ndani litakhubiriwa juu darini. 4 Lakini nawaambia ninyi rafiki zangu, Msiwaogope wao wauuao mwili na baada ya haya hawana neno la kutenda la zaidi. 5 Illa nitawaonya mtakaemwogopa: Mwogopeni yule aliye na uweza baada ya kuua mtu kumtupa katika Jehannum: naam, nawaambieni, Mwogopeni yule. 6 Haviuzwi videge vitano kwa pesa mbili? na hatta kimojawapo hakisahauliwi mbele ya Mungu: 7 walakini hatta nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope bassi: ninyi bora kuliko videge vingi. 8 Nami nawaambieni, Killa atakaenikiri mbele za watu, Mwana wa Adamu nae atamkiri mbele za malaika wa Mungu. 9 Nae aliyenikana mbele ya watu, atakanwa mbele za malaika wa Mungu. 10 Na killa mmoja atakaesema neno juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, bali yeye aliyemtukana Roho Mtakatifu hatasamehewa. 11 Na watakapowapeleka mbele za sunagogi na maliwali na wenye mamlaka, msifadhaike kwa kuwaza jinsi mtakavyojibu au mtakavyosema: 12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa hiyo hiyo yawapasavyo kuyanena. 13 Mtu mmoja katika makutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu. 14 Akamwambia, Ee mwana Adamu, nani aliyemweka kuwa kadhi au mgawanyi juu yenu? 15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na kutamani, maana uzima wa mtu hautoki katika mali zake, kwa sababu ana wingi wa mali. 16 Akawaambia mfano, akisema, Palikuwa na mtu tajiri, shamba lake likastawi. 17 Akaanza kuwaza moyoni, akisema, Nifanyeje, maana sina pa kuweka akiba mavuno yangu? 18 Akasema, Nitafanya hivi: nitavunja ghala zangu, nitajenga kubwa zaidi: na humo nitaweka akiba nafaka zangu zote, na mali zangu. 19 Kiisha nitaiambia roho yangu, Ee roho yangu, nna mali nyingi ulizojiwekea akiba kwa miaka mingi: pumzika, hassi, ule, unywe, ufurahi. 20 Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo, wanakutaka roho yako. Nayo uliyojiwekea tayari yatakuwa ya nani? 21 Ndivyo alivyo yeye ajiwekeae nafsi yake akiba wala hawi tajiri machoni pa Mungu. 22 Akawaambia wanafunzi wake, Kwa sababu hii nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mleni: wala miili yenu mvaeni. 23 Kwa maana maisha ni zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi. 24 Watafakarini kunguru, hawapandi wala hawavuni: hawana pa kuweka akiba wala ghala, na Mungu huwalisha. Ninyi si hora sana kuliko ndege? 25 Yupi wenu awezae kwa kusumbuka kujiongeza kimo chake mkono mmoja? 26 Bassi ikiwa hamwezi hatta neno lililo dogo, ya nini kujisumbulia mambo mengine? 27 Yatafakarini maua jinsi yameavyo: hayatendi kazi wala hayasokoti, nami nawaambieni ya kwamba hatta Sulemani, katika fakhari yake yote hakuvikwa kama mojawapo la hayo. 28 Bassi ikiwa Mungu huvika hivi haya majani ya kondeni yaliyopo leo, yakatupwa kalibuni kesho, si ninyi zaidi sana, enyi wa imani haba? 29 Bassi ninyi msitafute mtakavyokula wala mtakavyokunywa, wala msiwe na roho yenye tashwishi. 30 Maana mataifa wa dunia huyatafuta hayo yote, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo. 31 Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na haya yote mtazidishiwa. 32 Msiogope, enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapeni ufalme. 33 Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu. 34 Kwa maana hazina yenu ilipo ndipo na itakapokuwa na mioyo yenu. 35 Mwe, bassi, mmefungwa viuno, na taa zikiwaka; 36 na ninyi kama watu wanaomngojea bwana wao, atakapoondoka arusini, illi akija na kubisha, wamfungulie marra moja. 37 Wa kheri watumishi wale ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesba. Amin, nawaambieni, atajifunga, atawaketisha, atakuja kuwakhudumia. 38 Na akija kesha la pili au akija kesha la tatu, na kuwakuta hivi, wa kheri watumishi wale. 39 Lakini jueni haya ya kuwa mwenye nyumba angaliijua saa atakayokuja mwizi, angalikesha asiache nyumba yake kuvunjwa. 40 Na ninyi, bassi, mwe tayari, kwa sababu saa msiyodhani, Mwana wa Adamu yuaja. 41 Petro akasema, Bwana, unatuambia sisi mfano huu au watu wote pia? 42 Bwana akasema, Nani, bassi, aliye wakili mwaminifu niwenye busara, ambae Bwana wake atamweka juu ya ntumishi wake wote, awape watu posho lao kwa saa yake? 43 Yu kheri mtumishi yule ambae bwana wake ajapo atamkuta amefanya hivyo. 44 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya mali zake zote. 45 Bali mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja; akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume na wanawake, na kula na kulewa; 46 bassi, bwana wa mtumwa yule atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande vipande, atampa sehemu yake pamoja na wasioamini. 47 Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya Bwana wake, asijiweke tayari, wala kutenda mapenzi yake, atapigwa mapigo mengi; 48 na yule asiyejua, nae amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa mapigo machache. Killa aliyepewa vingi kwake huyu vitatakwa vingi: nae waliyemkabidhi vingi, kwake yeye watataka vingi zaidi. 49 Nimekuja kutupa moto duniani, na ukiwa umekwisha kuwashwa nataka nini zaidi? 50 Nina ubatizo wa kubatizwa nao, na nina dhiiki namna gani hatta utakapotimizwa! 51 Je! wadhani kwamba nimekuja niipe dunia amani? Nawaambieni, Sivyo, bali mafarakano. 52 Kwa maana tangu sasa katika nyumba moja watakuwa watu watano wamefarakana, watatu na wawili, na wawili na watatu. 53 Baba wa mtu atafarakana na mwanawe, na mwana na baba yake, mama ya mtu na binti yake, na binti na mama yake, mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu. 54 Akawaambia na makutano pia, Killa muonapo wingu likizuka magharibi, mwasema marra, Mvua inakuja. 55 Na killa ivumapo kaskazi mwasema, Itakuwa joto; ikawa. 56 Enyi wanafiki, mwajua kuufasiri uso wa inchi na mbingu; imekuwaje, bassi, hamjui kuyafasiri majira haya? 57 Na mbona ninyi katika nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? 58 Bassi, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa liwali, njiani ujitahidi kupatanishwa nae: asije akakukokota mbele ya kadhi, yule kadhi akakutia katika mikono ya askari, yule askari akakutupa gerezani. 59 Nakuambia, Hutoki humo kabisa hatta uishe kulipa roho pesa ya mwisho. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania