Luka 11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 IKAWA alipokuwa mahali fullani, anasali, alipokoma, mmoja katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali kama Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake. 2 Akawaambia, Msalipo, semeni: Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako takatifu litukuzwe. 3 Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe, kama mbinguni, kadhalika duniani. 4 Utupe leo riziki zetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa maana sisi nasi tunamsamehe killa mtu anaewiwa nasi. Usituingize majaribuni, hali utuokoe na yule mwovu. 5 Akawaambia, Nani kwenu aliye na rafiki akamwendea usiku wa manane akamwambia, 6 Ee rafiki, uniazime mikate mitatu: maana rafiki yangu amekuja kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kumwandikia. 7 Na yule mle ndani akamjibu, akimwambia, Usiniudhi: mlango umekwisha kufungwa, na watoto wangu wamelala pamoja nami kitandani; siwezi kuondoka nikupe. 8 Nawaambieni, Ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, illakini kwa kuwa yule hana haya ataondoka na kumpa yote ahitajiyo. 9 Nami nawaambia ninyi, Ombeni na mtapewa: tafuteni na mtapata: bisheni na mtafunguliwa. 10 Kwa sababu killa aombae hupewa: nae atafutae hupata: nae abishae hufunguliwa. 11 Kwa maana ni nani kwenu aliye baba, mwanawe akamwomba mkate, je! atampa jiwe? au akimwomba samaki, badala ya samaki atampa nyoka? 12 au akimwomba yayi, atampa nge? 13 Bassi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Baba aliye mbinguni, je! hatazidi na kuwapa wote wamwombao Roho Mtakatifu? 14 Na Yesu alikuwa akifukuza pepo bubu. Ikawa yule pepo alipotoka, bubu akasema, makutano wakastaajabu. 15 Wengine wao wakasema, Kwa Beelzebul, mkubwa wa pepo atoa pepo. 16 Wengine kwa kumjaribu wakataka ishara ya mbinguni. 17 Nae, akiyajua mawazo yao, akawaambia, Killa ufalme uliogawanyika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa, na nyumba iliyogawanyika nyumba kwa nyumba huanguka. 18 Nae Shetani vivyo hivyo akigawanyika katika nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? kwa maana ninyi mnasema ninafukukuza pepo kwa Beelzebul. 19 Lakini mimi nikifukuza pepo kwa Beelzebul, wana wenu huwafukuza kwa nani? bassi kwa hiyo hawo ndio watakaokuwa waamuzi wenu. 20 Lakini nikifukuza pepo kwa kidole cha Mungu, bassi ufalme wa Mungu umewajieni. 21 Aliye na nguvu, mwenye silaha zake, alindapo na wake, mali zake zimo katika amani: 22 lakini mwenye nguvu za kumpita yeye atakapokuja na kumshinda, amnyangʼanya silaha zake zote alizotegemea, na mateka yake ayagawanya. 23 Mtu asiye pamoja nami ni adui yangu: nae asiyekusanya pamoja nami hutapanya. 24 Pepo mchafu amtokapo mtu, hupita kati ya mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika: asipopata hunena, Nitarudi uyumbani kwangu nilikotoka. 25 Akija, huiona imefagiwa, imepambwa. 26 Marra huenda, huchukua pepo saba wengine walio waovu kupita nafsi yake: nao huingia na kukaa humo: na mambo ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. 27 Ikawa alipokuwa akinena haya, mwauamke mmoja katika makutano akapaaza sauti yake akamwambia, Li kheri tumbo lililokuehukua, na maziwa uliyonyonya. 28 Lakini yeye akasema, Bali afadhali wa kheri wenye kulisikia neno la Mungu na kulishika. 29 Makutano walipokuwa wakimkusanyikia akaanza kunena, Kizazi hiki ni kizazi kibaya: chatafuta ishara: wala hakitapewa ishara illa ishara ya nabii Yunus. 30 Maana kama vile Yunus alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa kwa kizazi hiki. 31 Malkia wa kusini atafufuliwa siku ile ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atawahukumu; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia illi kuisikia hekima ya Sulemani; na hapa pana khabari kubwa kuliko Sulemani. 32 Watu wa Ninawi watasimama siku ile ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao wataihukumu: maana wao walitubu kwa ajili ya makhubiri ya Yunus, na hapa pana khabari kubwa kuliko Yunus. 33 Hapana mtu awashae taa na kuiweka mahali pa siri au chini va pishi, bali huiweka juu ya kibao cha kuwekea taa: illi waingiao wanone mwanga. 34 Taa ya mwili ni jicho, bassi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote nna nuru, lakini jicho lako likiwa ovu, mwili wako nao una giza. 35 Angalia bassi, ile nuru iliyo ndani yako isije ikawa giza. 36 Bassi, kama mwili wako wote nna nuru, tena kama hanna sehemu iliyo na giza, mwili wako utakuwa na nuru kabisa kama vile taa ikumulikiavyo kwa mwangaza wake. 37 Hatta alipokuwa akisema, Farisayo mmoja akamwita ale chakula cha assubuhi kwake: akaingia, akaketi. 38 Yule Farisayo alipoona akastaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula. 39 Bwana akamwambia, Sasa ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sabani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyangʼanyi ua uovu. 40 Enyi wapumbavu, yeye aliyekifauya cha nje, siye aliyekifanya cha ndani naebo? 41 Lakini toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vitu vyote ni safi kwemi. 42 Bali ole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnalipa zaka za mnaana na mchicha, na killa mboga, mkaacha adili na upendo wa Mungu: iliwapaseni kuyafanya haya ya kwanza bila kuacha haya ya pili. 43 Ole wenu, Mafarisayo, kwa sababu mwapenda kukaa mbele katika sunagogi na kusalimiwa masokoni. 44 Ole wenu, maana mfano wenu ni makaburi yasiyoonekana, na watu wapitao juu yao hawana khabari. 45 Mtu mmoja katika wana sharia akajibu, akamwambia, Mwalimu, ukisema haya watushutumu sisi nasi. 46 Akasema, Na ninyi wana sharia, ole wenu, kwa sababu mwawachukuza watu mizigo isiyochukulika, na ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo kwa kimojawapo cha vidole vyenu. 47 Ole wenu kwa sababu mnajenga makaburi ya manabii, na baba zenu waliwaua. 48 Hivyo ndivyo mnavyoshuhudia matendo ya baba zenu na kupendezwa nayo: maana wao waliwaua, na ninyi mnajenga makaburi yao. 49 Na kwa hiyo hekima ya Mungu ilisema, Nitatuma kwao manabii na mitume, na wataua baadhi yao, na kuwaudhi, 50 illi kwa kizazi hiki itakwe damu ya manabii wote ilivomwagika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu; 51 tangu damu ya Habil hatta damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhhahu na patakatifu. Naam, nawaambieni, itatakwa kwa kizazi hiki. 52 Ole wenu, enyi wana sharia, kwa sababu mliuchukua ufunguo wa maarifa; ninyi wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mliwazuia. 53 Alipokuwa akiwaambia haya, waandishi na Mafarisayo wakaanza kumsonga vibaya, na kumchokoza kwa masiala mengi, wakimwotea, 54 wakitaka kudaka neno kinywani mwake wapate kumshitaki. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania