Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI baada ya mambo haya Bwana akachagua wengine sabaini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda killa mji na pahali atakakokwenda mwenyewe.

2 Akawaambia, Mavuno ni mengi, illakini watenda kazi wachache; mwombeni, bassi, Bwana wa mavuno, apate kupeleka watenda kazi mavunoni mwake.

3 Enendeni: angalieni, nakutumeni ninyi kama wana kondoo kati ya mbwa wa mwitu.

4 Msichukue kifuko, wala mkoba, wala viatu: wala msimsalimu mtu njiani.

5 Na nyumba yo yote mwingiayo, kwanza neneni, Amani iwe nyumbani humu.

6 Na kama yumo mwana wa amani, amani yenu itakaa kwake. La! si hivyo, itawarudia ninyi.

7 Kaeni katika nyumba hiyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; kwa maana mtenda kazi astahili kupewa ijara yake.

8 Msihame nyumba kwa nyumba. Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisheni, vileni vitu vile viwekwavyo mbele yenu.

9 Waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni ya kama, Ufalme wa Mungu umewakaribieni.

10 Na mji wo wote mtakaouingia nao hawawakaribishi utokeni, mkipita katika njia zake semeni,

11 Hatta mavumbi haya ya mji wenu, yaliyogandamana nasi, twayakungʼuta juu yenu: illakini jueni haya, ya kuwa ufalme wa Mungu umewakaribieni.

12 Nawaambieni, itakuwa rakhisi Sodoma istahimili adhabu yake siku ile kuliko mji ule.

13 Ole wako, Korazin! Ole wako Bethsaida! kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingalifanyika katika Turo na Sodom, wangalitubu zamani, wakiketi katika nguo za kigunia na majivu.

14 Lakini itakuwa rakhisi Turo na Sidoni istahimili adhabu zao siku ile ya hukumu, kuliko ninyi.

15 Nawe Kapernaum, wewe uliyeinuliwa hatta mhinguni, ntashushwa hatta kuzimu.

16 Awasikiae ninyi, anisikia mimi, nae awakataae ninyi, anikataa mimi; nae anikataae mimi amkataa yeye aliyenituma.

17 Wale sabaini wakarudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hatta pepo wanatutii kwa jina lako.

18 Akawaambia, Nalimwona Shetani kama umeme akianguka toka mbinguni.

19 Tazameni, nawapeni mamlaka va kuwakanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hapana kitu kitakachowadhuru ninyi kamwe.

20 Lakini msifurahi kwa sababu hii ya kuwa pepo wanawatiini: hali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni.

21 Saa ileile Yesu akashangilia katika Roho, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na busara mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga: Naam, Baba, kwa maana ndivyo vilivyokuwa vinapendeza mbele yako.

22 Akawagenkia wanafunzi wake akasema, Nimekahidhiwa vyote na Baba yangu: wala hapana mtu ajuae khabari za Mwana illa Baba: wala khabari za Baha illa Mwana, na mtu ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia.

23 Akawageukia wanafunzi wake kwa faragha, akawaambia, Ya kheri macho yatazamayo mnayoyatazama ninyi.

24 Maana nawaambia; Manabii wengi na wafalme walitaka kuyaona mnayoyatazama ninyi wasiyaone, na kuyasikia mnayoyasikia wasiyasikie.

25 Mwana sharia mmoja akasimama akimjaribu, akasema, Mwalimu, nifanyeni niurithi uzima wa milele?

26 Akamwambia, Katika torati imeandikwa nini? Wasomaje?

27 Nae akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi, ndipo utaishi.

29 Nae akitaka kujifanya ana haki akamwambia Yesu, Na jirani yangu ni nani?

30 Yesu akajibu akasema, Kulikuwa na mtu akishuka kutoka Yerusalemi kwenda Yeriko; akaangukia katika mikono ya wanyangʼanyi, wakamvua nguo zake, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakamwacha nussu ya kufa.

31 Na kwa nasibu kukashuka kuhani mmoja njia ileile, akamwona, akapita upande.

32 Na Mlawi kadhalika alipofika pahali pale, akamwona akapita upande.

33 Lakini Msamaria mmoja akisafiri, akamjia, nae alipomwona akamhurumia;

34 bassi akamjongelea, akamfunga jeraha zake, akitia mafuta na mvinyo: akampandisha juu ya nyama wake, akamleta katika nyumba ya wageni, akamwuguza.

35 Hatta assubuhi yake akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba, akasema, Mwuguze: na cho chote utakachogharimia zaidi, nirudipo, nitakulipa.

36 Waonaje bassi? Katika hawa watatu yupi aliyekuwa jirani yake mwenye kuangukia katika mikono ya wanyangʼanyi?

37 Akasema, Ni yule aliyemfanyia huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye kama hayo.

38 Nao walipokuwa wakienenda, akaingia katika kijiji kimoja; na mwanamke mmoja, jina lake Martha, akamkaribisha nyumbani mwake.

39 Nae alikuwa na ndugu mwanamke aitwae Mariamu, nae alikuwa ameketi miguuni pa Yesu, akasikia maneno yake.

40 Bali Martha alihangaika kwa khuduma nyingi: akamwendea, akasema, Bwana, haikukhussu wewe ya kuwa ndugu yangu ameniacha kukhudumu peke yangu? Bassi mwambie anisaidie.

41 Bwana akamjibu akamwambia, Martha, Martha, unajisumbua na kujifadhaisha kwa ajili ya mambo mengi:

42 lakini kuna haja ya kitu kimoja tu, na Mariamu ameichagua sehemu iliyo njema, ambayo hataondolewa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo