Luka 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KWA kuwa wiitu wengi wametia mkono kutunga khabari za mambo yale yaliyotimizwa kati yetu, 2 kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi, ua watumishi wa lile neno tokea mwanzo, 3 nimeona vema na mimi, nikiisha kujipatia khabari zilizo sahihi za mambo yote tokea awali, kukuandikia kwa taratibu. Theofilo il-aziz: 4 upate kujua usahihi wa maneno yale uliyofundishwa. 5 Zamani za Herode, mfalme wa Yahudi, palikuwa na kuliani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya: na mkewe alikuwa mmojawapo wa binti Haruni, jina lake Elizabeti. 6 Nao wote wawili wenye haki mbele ya Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na hukumu zake zote bila lawama. 7 Nao walikuwa hawana mtoto; maana Elizabeti alikuwa tassa, nao wote wawili wazec sana. 8 Bassi ikawa alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele ya Mungu, 9 kama ilivyokuwa desturi ya ukubani, kura ikamwangukia kuingia katika hekalu la Bwana, na kufukiza uvumba. 10 Na mkutano wote wa watu walikuwa wakisali nje, saa ya kufukiza. 11 Akatokewa na Malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhbahu ya kufukizia. 12 Zakaria akafadhaika alipomwona, khofu ikamwingia. 13 Yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mke wako Elizabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. 14 Nawe utakuwa na furaha na shangwe; na watu wengi watafurahia kuzaliwa kwake. 15 Kwa maani atakuwa mkuu mbele ya Mungu, hatakunywa divai wala kileo: nae atajazwa Roho Mtakatifu hatta tangu tumbo la mama yake. 16 Na wengi katika wana wa Israeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. 17 Nae atatangulia mbele ya uso wake, mwenye roho ya Eliya, na nguvu zake, kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na kuwageuza maasi waelekee akili zao wenye haki; illi kumfanyia tayari Bwana watu waliotengenezwa. 18 Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje hayo? Maana mimi mzee na mke wangu kongwe wa siku nyingi. 19 Malaika akamjibu, akamwambia, Mimi ni Gabrieli nisimamae mbele ya Mungu: nami nalitumwa niseme nawe, na kukupasha khabari hizi njema. 20 Nawe utakuwa bubu, usiweze kusema hatta siku ile yatakapotokea hayo: kwa sababu hukusadiki maneno yangu: nayo yatatimizwa wakati wake. 21 Na wale watu walikuwa wakimugojea Zakaria, wakastaajabu kwa kukawia kwake mle hekaluni: 22 hatta alipotoka hakuweza kusema nao, wakatambua ya kuwa ameona maono mle hekaluni; nae alikuwa akiwapungia mkouo, akadumu kuwa bubu. 23 Ikawa siku za khuduma yake zilipotimia, akaenda zake nyumbani kwake. 24 Hatta baada ya siku zile mkewe Elizabeti akachukua mimba akajificha miezi mitano, akisema, 25 Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana, siku zile alizoniangalia, kuniondolea aibu yangu mbele ya watu. 26 Mwezi wa sita malaika Gabrieli alipelekwa na Mungu kwenda mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, 27 kwa mwanamke bikira aliyekuwa ameposwa na mume, jina lake Yusuf, wa nyumba ya Daud; na jina la yule mwanamke Mariamu. 28 Akaja kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. 29 Nae akafadhaika kwa khabari ya neno hili, akawaza moyoni mwake, Hii ni salamu gani? 30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu; kwa maana umepata neema kwa Mungu. 31 Tazama, utachukua mimba, utazaa mwana, utamwita jina lake Yesu. 32 Huyu atakuwa mkuu, atakwitwa Mwana wake Aliye juu; na Bwana Mungu atampa kiti cha Daud baba yake. 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hatta milele; wala ufalme wake hautakuwa na mwisho. 34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili; kwa maana simjui mume? 35 Malaika akajibu, akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia, na nguvu zake Aliye juu zitakutilia kivuli: kwa biyo kitakachozaliwa kitakwitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. 36 Na tazama, nae Elizabeti jamaa yako, ana mimba ya mtoto mume katika uzee wake: na mwezi hun wa sita kwake yeye aliyekwitwa tassa: 37 kwa maana hapana neno lisilowezekana kwa Mungu. 38 Mariamu akasema, Tazama, mimi mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kwa neno lako. Malaika akaondoka kwake. 39 Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda milimani kwa haraka hatta mji mmoja wa Yuda. 40 Akaingia nyumbani kwa Zakaria, akamwamkia Elizabeti. 41 Ikawa Elizabeti alipoisikia salamu ya Mariamu, mtoto mchanga akaruka ndani ya tumbo lake; Elizabeti akajazwa Roho Mtakatifu, akapaaza sauti yake kwa nguvu, akasema, 42 Umebarikiwa wewe katika wanawake, na uzao wa tumbo lako umebarikiwa. 43 Na latoka wapi neno hili lililonipata, mama wa Bwana wangu anijilie mimi? 44 Kwa maana sauti ya salamu yako ilipoingia masikioni mwangu, mtoto mchanga aliruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu. 45 Na yu kheri aliyesadiki, kwa maana maneno hayo aliyoambiwa na Bwana yatatimizwa. 46 Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, 47 Roho yangu yamfurahia Mungu, Mwokozi wangu. 48 Kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake: Kwa maana hakika, tokea leo vizazi vyote wataniita kheri. 49 Kwa kuwa aliye hodari amenitendea makuu; Na Jina lake ni takatifu. 50 Na rehema zake vizazi hatta vizazi Kwao wanaomcha. 51 Ametenda nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mioyo yao. 52 Amewashusha wakuu katika viti, Amewakweza wanyonge. 53 Wenye njaa amewashibisha mema; Wenye mali amewaondoa mikono mitupu 54 Kwa kukumbuka rehema Amemsaidia Israeli mtumishi wake, 55 (Kwa jinsi alivyowaambia baba zetu) Ibrahimu na nzao wake, hatta milele. 56 Mariamu akakaa nae kadri ya miezi mitatu, akarudi nyumbani kwake. 57 Hatta Elisabeti akatimiziwa wakati wake wa kuzaa, akazaa mwana mume. 58 Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake; wakafurahiwa pamoja nae. 59 Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babae, Zakaria. 60 Akajibu mamae, akasema, Sivyo, lakini atakwitwa Yohana. 61 Wakamwambia, Hapana mtu katika jamaa zako aitwae jina hilo. 62 Wakamwashiria babae, kumwuliza atakaje aitwe. 63 Akataka kibau, akaandika, akanena, Yohana ni jina lake. Wakataajabu wote. 64 Marra akafunguliwa kinywa na ulimi wake, akanena, akimbariki Mungu. 65 Khofu ikawaingia wote waliokaa karibu nao; yakaenea maneno haya pia milimani mwote Uyahudi. 66 Na wote waliosikia wakayaweka mioyoni mwao, wakinena, Mtoto gani bassi atakuwa huyu? Kwa maana mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nae? 67 Zakaria babae akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akinena, 68 Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli; Kwa kuwa amewajia watu wake na kuwakomboa. 69 Ametuondokeshea wokofu wa nguvu Katika nyumba ya Daud mtumishi wake. 70 (Kama alivyosema kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu mwanzo), 71 Tuokolewe na adui zetu, na katika mikono yao wote wauaotuchukia; 72 Illi kuwatendea rehema baba zetu, Na kukumbuka agano lake takatifu; 73 Uapo aliomwapia Ibrahimu baba yetu, 74 Ya kwamba atatupa sisi, tukiokoka mikononi mwa adui zetu, tumwabudu pasipo khofu, 75 Katika utakatifu na kwa haki mbele zake siku zetu zote. 76 Na wewe nawe, Mtoto, utakwitwa nabii wake Aliye juu: Kwa maana utatangulia mbele ya uso wake Bwana ufanyize njia zake; 77 Uwajulishe watu wake wokofu Zikiondolewa dhambi zao, 78 Kwa rehema zake Mungu wetu, Kwazo mwangaza wa juu umetujia, 79 Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuelekeza miguu yetu mnamo njia ya amani. 80 Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu rohoni; akawako majangwani hatta siku ya kutokea kwake kwa Israeli. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania