Filemoni 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 PAOLO, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yelu, kwa Filemon mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi, 2 na kwa Appia, ndugu yetu mpendwa, na kwa Arkippo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako; 3 Neema lwe nanyi na amani zitokazo kwa Mungu, baba yetu, tta kwa Bwana Yesu Kristo. 4 Namshukuru Mungu wangu, siku zote nikikukumbuka katika maombi yangu, 5 nikisikia khabari ya upendo wako na ya imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote; 6 illi ushirika wa imani yako ufanye kazi yake katika ujuzi wa killa kitu chema kilicho kwenu katika Kristo Yesu. 7 Maana tuna furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu lmeburudishwa nawe, ndugu. 8 Kwa hiyo, nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasalo; 9 illakini, kwa ajili ya upendo, nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paolo mzee, na sasa mfungwa wa. Yesu Krlsto pia. 10 Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika mafungo yangu, Onesimo, 11 ambae zamani allkuwa hakufai, hali sasa akufaa saua, wewe na mimi pia; 12 niliyemtuma kwako, nawe umkubali, maana ni moyo wangu; 13 ambae mimi nalimtaka akae nami, apate kunikhudumia hadala yako katika mafungo ya Injili; 14 lakini slkutaka kuteuda neno isipokuwa kwa shauri lako, illi wema wako usiwe kama kwa shuruti, hali kwa khiari yako. 15 Maana, labda ndio sababu alitengwa nawe muda kitambo illi uwe nae tena milele; 16 tokea sasa, si kama mtumwa, baii lieha ya mtumwa, ndugu mpendwa, kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana. 17 Bassi kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama mimi. 18 Na kama amekudhulumu, au awiwa nawe kitu, ukiandike juu yangu. 19 Mimi Paoio nimeandika kwa mkouo waugu mweuyewe, nitalipa. Sikuambii kwamba wawiwa nami hatta nafsi yako. 20 Naam, ndugu yangu, nipate faida kwako katika Bwana; uniburudishe moyo waugu katika Kristo. 21 Nikiamini kutii kwako nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo. 22 Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa: maana nataraja ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata. 23 Epafra, aliyefuugwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu; 24 na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami. 25 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania