2 Wathesalonike 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 BASSI tunakusihini, ndugu, katika khabari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele yake, 2 msifadhaishwe upesi na kuaeha nia yenu, wala msistushwe, kwa roho wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, ya kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo. 3 Mtu aliye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana haiji isipokuja kwanza ile faraka, akafumiliwa yule mtu wa dhambi, mwana wa uharibifu, 4 yule mpingamizi, ajiinuae nafsi yake juu ya killa kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hatta yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu, kama Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba ndive Mungu. 5 Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwa pamoja nanyi naliwaambieni hayo? 6 Na sasa lizuialo mwalijua, apate kufunuliwa huyu wakati wake. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; 7 lakini yuko azuiae sasa, hatta atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake; 9 ambae kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kazi kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za nwongo, 10 na katika madanganya yote ya udhalimu kwao wanaopotea: kwa sababu hawakukubali kuipenda kweli, wapate kuokolewa. 11 Kwa biyo Mungu atawaletea nguvu ya upotevu, wauamini uwongo, 12 illi wahukumiwe wote wasioamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. 13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokofu, katika kutakaswa kwa Roho na kuiamini kweli, 14 aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, illi kuupata ntukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. 15 Bassi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ikiwa kwa maneno, au kwa waraka wetu. 16 Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, 17 awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika killa neno na tendo jema. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania