2 Wathesalonike 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 PAOLO, Silwano, na Timotheo kwa kanisa la Wathessaloniki lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo: 2 Neema iwe kwenu na imani zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo. 3 Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi. 4 Hatta sisi wenyewe twajisifu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya uvumilivu wenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na mateso mnayoyavumilia; 5 ndio ishara ya hukumu ya haki ya Mungu illi mstabilishwe kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa; 6 kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi, 7 na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake, 8 katika mwako wa moto, akiwalipa kisasi wao wasiomjua Mungu, nao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo; 9 watakaoadhibiwa kwa uharibifu wa milele, kutengwa na uso wa Bwana na na utukufu wa nguvu zake, 10 atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile. 11 Kwa hiyo twawaombea ninyi siku zote, illi Mungu wetu awahesabu kuwa nimeustahili wito wenu, akatimize killa haja ya wema na killa kazi ya imani kwa nguvu: 12 jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe kwenu, na ninyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania