Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Wakorintho 9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA khabari za kuwakhudumia watakatifu sina haja ya kuwaandikia.

2 Maana najua utajiri wenu, niliojisifia kwa Wamakedoni, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo watu wengi.

3 Lakini naliwatuma ndugu, illi kujisifu kwangu kwa ajili yenu kusibatilike katika jambo hili; mpate kuwa tayari, kama nilivyosema:

4 kusudi, wakija Wamakedoni pamoja nami, na kuwakuta hamjawa tayari, tusije tukatahayarika sisi, tusiseme ninyi, katika hali hii va kutumaini.

5 Bassi naliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, illi iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa choyo.

6 Lakini nasema neno liili, Apandae haha atavuna haha; apandae kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.

7 Killa mtu na atende alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoae kwa moyo wa ukunjufu.

8 Na Mungu aweza kuwajaza killa neema kwa wingi, illl ninyi, mkiwa na riziki za killa namna siku zote, mpate kuzidi sana katika killa tendo jema;

9 kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.

10 Na yeye amruzukuye mbegu mwenye kupanda, atoae mkate uwe chakula, atawapeni mbegu za kupanda na kuzizidisha, atayaongeza mazao ya haki yenu;

11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.

12 Maana utumishi wa khuduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;

13 kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huu, mnamtukuza Mungu kwa ajili ya ntii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.

14 Nao wenyewe, wakiwaombea ninyi, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sanu ndani yenu.

15 Mungu ashukuriwe kwa sababa ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu ipasavyo.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo