Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Wakorintho 8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 TENA twawaarifu ninyi, ndugu, kliahari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia;

2 maana walipokuwa wakijaribiwa kwa shidda nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa unyofu wao.

3 Maana nawashuhudia, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao,

4 kwa khiari yao wenyewe walitoa vitu vyao; wakituomba pamoja na kutusihi tuipokee neema hii, na kushirikiana nao huku kuwakhudumia watakatifu.

5 Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini, bali kwanza walijitoa nafsi zao, wakampa Bwana; kiisha wakatupa sisi pia, kwa mapenzi ya Mungu,

6 hatta tukamwonya Tito kuwatimilizieni neema hii kama vile alivyoianza.

7 Lakini kama mlivyo na wingi wa vitu vyote, imani, na matamko, na elimu, na bidii yote, na mapenzi yenu kwetu sisi; bassi vivyo hivyo mwe na wingi wa neema hii pia.

8 Sineni illi kuwaamuru, bali kwa bidii ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu.

9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, illi ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.

10 Nami katika neno hili natoa shauri langu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, wapata mwaka, licha ya kutenda hivi, hatta kutaka pia.

11 Lakini sasa mkatimize kule kutenda nako, illi kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mwe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.

12 Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.

13 Maana sisemi haya, illi wengine waachiliwe ninyi mkalemewe,

14 bali mambo yawe sawa sawa: wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, illi na wingi wao uwafae ninyi upungufu wenu; illi mambo yawe sawa sawa.

15 Kama ilivyoandikwa, Aliyekusanya vingi, hakuzidi, nae aliyekusanya vichache hakupungukiwa.

16 Lakini Mungu ashukuriwe atiae bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito.

17 Maana alipokea yale maonyo; nae, akizidi kuwa na bidii, alisafiri kwenda kwenu kwa khiari yake mwenyewe.

18 Na pamoja nae tukamtuma ndugu yule ambae sifa zake katika Injili zimeenea makanisani mwote.

19 Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nias katika jambo la neema hii inayokhudumiwa nasi, illi Bwana atukuzwe, ikadhihirike ya kuwa mioyo yenu ilikuwa tayari.

20 Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu katika khabari ya karama hii inayokhudumiwa nasi;

21 tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele ya Bwana tu, bali na mbele ya wana Adamu.

22 Nasi pamoja nae tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona katika mambo mengi kuwa ana bidii, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini alilo nalo kwenu.

23 Bassi mtu akitaka khabari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami; tena akitaka khabari za ndugu zetu, wao ni mitume ya makanisa, na utukufu wa Kristo.

24 Bassi waonyesheni mbele ya makanisa bayana ya upendo wenu, na ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo