Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Wakorintho 7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu.

2 Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu, hatukumharibu mtu, hatukumkalamkia mtu.

3 Sisemi neno hili illi niwahukumu ninyi; kwa maana nimetangulia kusema ya kwamba ninyi m katika mioyo yetu mpaka kufa pamoja, na kuishi pamoja.

4 Nina ujasiri mwingi kwemi; kujisifu kwangu kwa ajili yenu ni kwingi. Nimejawa na faraja, katika mateso yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.

5 Kwa maana hatta tulipokuwa tumelikia Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tuliteswa kote kote; nje palikuwa na vita, ndani khofu.

6 Illakini Mungu, mwenje kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuwapo kwake Tito.

7 Wala si kwa kuwapo kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu khabari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hatta nikazidi kufurahi.

8 Maana ijapokuwa naliwahuzunisha kwa waraka ule sijuti, ijapokuwa nalijuta; maana naona ya kwamba waraka ule nliwahuzunisha, ijapokuwa ni kwa kitambo.

9 Sasa nafurahi, si kwa sababu ya kuhuzunishwa ninyi, bali kwa sababu mlihuzunishwa hatta mkatuhu. Maana mlihuzunishwa mmele za Mungu, msipate khasara kwa tendo letu katika neno lo lote.

10 Maana huzuni iliyo mbele za Mungu hufanyiza toba iletayo wokofu isiyo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanyiza mauti.

11 Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko mbele za Mungu kwalitenda bidii ya namna gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na khofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi. Kwa killa njia mmejionyesha kuwa safi katika jambo hilo.

12 Bassi, ijapokuwa naliwaandikia, sikuandika kwa ajili yake yeye aliyedhulumu, wala si kwa ajili yake aliyedhulumiwa, bali ijtihadi yenu kwa ajili yetu ipate kudhihirishwa kwenu mbele za Mungu.

13 Kwa hiyo tulifarijiwa; na katika kufarijiwa kwetu tulifurahi sana kupita kiasi kwa sababu ya furaha ya Tito; maana roho yake imeburudishwa na ninyi nyote.

14 Kwa maana, ikiwa nimejisifu kwake kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; hali, kama tulivyowaambieni mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.

15 Na mapenzi yake kwenu yamekuwa mengi kupita kiasi, akumbukapo kutii kwenu ninyi nyote, jinsi mlivyomkaribisha kwa khofu na kutetemeka.

16 Nafurahi, kwa sababu katika killa neno nina moyo mkuu kwa ajili yenu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo