2 Wakorintho 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KWA maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia ikiharibiwa, tuna jengo litokalo kwa Mungu, nyumha isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele katika mbingu. 2 Maana na sisi katika hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa vazi jingine, yaani kao letu litokalo mbinguni; 3 ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. 4 Kwa maana sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, hali kuvikwa vazi jingine, illi kitu kile kipatwacho na mauti kimezwe na uzima. 5 Bassi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lili hili ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho. 6 Bassi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali ya Bwana. 7 Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona. 8 Lakini tuna moyo mkuu; na tunaona vema zaidi kutoka katika mwili na kukaa pamoja na Bwana. 9 Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye. 10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo, illi killa mtu apokee kadiri alivyotenda kwa mwili, vikiwa vyema au vikiwa vibaya. 11 Bassi tukiijua khofu ya Bwana, twawavuta wana Adamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tunadhihirishwa katika dhamiri zenu pia. 12 Maana hatujisifu nafsi zetu mbele yenu marra ya pili, bali tukiwapeni sababu ya kujisifu kwa ajili yetu, illi mpate kuwa nayo mbele yao wanaojisifu kwa mambo ya nje tu, wala si kwa mambo ya moyoni. 13 Maana ikiwa tumerukwa na akili zetu, ni kwa ajili ya Mungu; au ikiwa tunazo akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu. 14 Maana upendo wa Kristo watulazimisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba ikiwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, bassi walikufa wote; 15 tena alikufa kwa ajili ya wote, illi walio hayi wasiwe hayi kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao. 16 Hatta imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awae yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemjua Kristo kwa jinsi ya mwili, sasa lakini hatumjui hivi tena. 17 Hatta imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya, vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya. 18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, nae alitupa khuduma ya upatauisho; 19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; nae ametia ndani yetu neno la upatanisho. 20 Bassi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anakusihini kwa vinywa vyetu: twawaombeni kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. 21 Maana alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili vefu, illi sisi tuwe haki ya Mungu katika Yeye. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania