2 Wakorintho 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KWA sababu hiyo, kwa kuwa tuna khuduma hii, kwa jinsi tulivyorehemiwa, hatulegei; 2 lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyosetirika, wala hatuenendi kwa ujanja, wala kulichanganya neno la Mungu na uwongo; hali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mhele za Mungu. 3 Ijapokuwa injili yetu imesetirika, imesetirika kwao wanaopotea; 4 ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. 5 Kwa maana hatujikhubiri nafsi zetu, hali Kristo Yesu Bwana; na sisi wenyewe kuwa watumishi wenu kwa ajili ya Kristo. 6 Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. 7 Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, illi adhama ya uwezo iwe ya Mungu, wala si yetu sisi. 8 Pande zote twasongwa, bali hatudhiikiki; twaona mashaka, hali hatukati tamaa; twaudhiwa, hali hatuachwi; 9 twatupwa chini, bali hatuangamizwi; 10 siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, illi uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu. 11 Maana sisi tulio hayi siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, illi uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu ipatwayo na manti. 12 Bassi hapo mauti hufanya kazi yake ndani yetu, hali nzima ndani yenu. 13 Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani, kama ilivyoandikwa. Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena; 14 tukijua kama yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua na sisi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi. 15 Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, illi, neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao wengi mashukuru yazidishwe, Mungu akatukuzwe. 16 Kwa hiyo hatuzimii; bali ijapokuwa mtu wetu wa nje unaharibiwa, illakini mtu wetu wa ndani unafanywa npya siku baada ya siku. 17 Maana mateso mepesi yetu, yaliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele ulio mwingi sana zaidi; 18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania