Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Wakorintho 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 LAKINI nafsini mwangu nalikusudia hivi, nisije kwenu tena kwa huzuni.

2 Maana mimi nikiwatia huzuni, hassi ni nani anifurahishae illa yeye ahuzunishwae nami?

3 Nami naliwaandikia neno lili hili, illi, nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumainia ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia.

4 Maana katika shidda nyingi na dhiiki ya moyo niliwaandikieni nikitoka machozi mengi; si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu nilio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi.

5 Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi, bali kwa sehemu ninyi nyote, nisije nikawalemea.

6 Yamtosha mtu wa jinsi hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi;

7 hatta, kiuyume cha hiyo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyu asije akatoswa katika huzuni ipitayo kiasi.

8 Kwa hiyo nawasihi kumthubutishia upendo wenu.

9 Maana naliandika kwa sababu hii pia, illi nipate bayana kwenu kwamba m wenye kutii katika mambo yote.

10 Maana kama mkimsamehe mtu lo lote, na mimi; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo,

11 Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana sisi si wajinga, tunajua fikara zake.

12 Bassi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo nikafunguliwa mlango katika Bwana,

13 sikupata raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia.

14 Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu.

15 Kwa maana sisi tu manukato va Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;

16 katika hao wa kwanza manukato ya mauti yao waendao hatta mauti; katika hao wengine manukato ya uzima wao waendao hatta uzima. Na nani atoshae kwa mambo haya?

17 Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo