Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Wakorintho 13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HII ndio marra ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu killa neno litathubutishwa.

2 Nimetangulia kuwaambia: na kama vile nilipokuwapo marra ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo natangulia kuwaambia wao waliofanya dhambi zamani, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia:

3 kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemae ndani yangu, ambae si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu.

4 Maana, ijapokuwa alisulibiwa katika udhaifu, illakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; bali tutaishi pamoja nae kwa uweza wa Mungu ulio ndani yenu.

5 Jijaribuni nafsi zenu kwamba m katika imani; jithubutisheni nafsi zenu. Au bamjijui nafsi zenu, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu isipokuwa mmekataliwa?

6 Lakini natumaini kama mtajua ya kuwa sisi hatukukataliwa.

7 Na namwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, bali ninyi mfanye lililo jema, tujapokuwa sisi kama waliokataliwa.

8 Maana hatuwezi kutenda neno kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli.

9 Maana twafurahi, sisi tulipo dhaifu, na ninyi hodari. Tena twaomba hili nalo, mtimilike.

10 Kwa biyo, naandika liayo nisipokuwapo, illi, nikiwapo, nisitumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana illi kujenga wala si kubomoa.

11 Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.

12 Salimianeni kwa busu takatifu.

13 Walio watakatifu wote wawasalimu.

14 Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo