Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Wakorintho 10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NAMI Paolo, nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo, mimi niliye mnyenyekevu niwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo mwenye ujasiri kwenu;

2 naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhani ya kuwasisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili.

3 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;

4 maana silaha za vita yetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu kuangusha ngome;

5 tukiangusha mawazo na kiila kitu kilichoinuka, kijiinuacho jun ya elimu ya Mungu; na tukifanya mateka fikara zote zipate kumtii Kristo:

6 tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia.

7 Je! mnayaangalia yaliyo mbele ya macho yenu? Mtu akijitumainia nafsi yake ya kuwa yeye ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi tu watu wa Kristo.

8 Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga ninyi wala si kuwaangusha), sitatahayarika;

9 nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu.

10 Maana wasema, Nyaraka zake nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini yu dhaifu, na maneno yake hayawi kitu.

11 Mtu kama huyu na afikiri hivi, ya kwamba jinsi tulivyo kwa maneno katika nyaraka tusipokuwapo, ndivyo tulivyo kwa matendo tukiwapo.

12 Maana hatuthubutu kujihesabu pamoja nao wenye kujisifu nafsi zao, wala kujilinganisha nao: bali wao wakijipima nafsi zao na nafsi zao na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili.

13 Lakini sisi hatutajisifu zaidi ya kadiri yetu; bali kwa kadiri ya cheo tulichopimiwa na Mungu, yaani kadiri ya kufika hatta kwenu.

14 Maana hatujitanui nafsi zetu kupita kadiri yetu, kana kwamba hatuwafikii ninyi; maana tulifika hatta kwenu katika injili ya Kristo;

15 wala hatujisifu zaidi ya kadiri yetu, katika kazi za watu wengine; bali tukiwa na tumaini ya kwamba, imani yenu ikuapo, tutakuzwa kwenu kwa kadiri yetu;

16 na kupata ziada hatta kuikhuhiri Injili katika inchi zilizo mpaka mmoja na inchi zenu; tusijisifu katika cheo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa.

17 Lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kukatika Bwana.

18 Maana mtu mwenye kubaliwa si yeye ajisifuye, hali yeve asifiwae na Bwana.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo