Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Wakorintho 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timothieo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, pamoja na watakatifu wote walio katika inchi yote ya Akaia:

2 Neema iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

3 Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;

4 atufarijiye katika shidda zetu zote illi tupate kuwafariji wale walio katika shidda za namna zote, kwa faraja tunazofarijiwa na Mungu.

5 Kwa kuwa vile vile kama mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo.

6 Lakini ikiwa sisi tu katika shidda, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokofu wenu, ufanyao kazi yake kwa kuvumilia mateso yale yale tuteswayo na sisi: au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokofu wenu.

7 Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa vile vile kama mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo m washiriki wa zile faraja.

8 Maana hatupendi, ndugu, msijue khabari ya shidda ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hatta tukakata tamaa ya kuishi.

9 Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu, illi tusijitumainie nafsi zetu, hali Mungu, awafufuae wafu, aliyetuokoa sisi na mauti kuu namna ile, tena ataokoa;

10 ambae tumemtumainia kwamba atazidi kutuokoa;

11 ninyi nanyi mkisaidiana kwa ajili yetu katika kuomba, illi, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa kazi ya watu wengi, watu wengi watoe mashukuru kwa ajili yetu.

12 Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.

13 Maana hatuwaandikii ninyi neno, illa yale msomayo, au kuyakiri; nami nataraja ya kuwa mtayakiri hatta mwisho;

14 vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana Yesu.

15 Na nikiwa na timiaini hilo nalitaka kwenda kwenu hapo kwanza, illi mpate karama ya pili;

16 na kupita kwenu na kuendelea hatta Umakedoni; na tena toka Makedonia kurudi kwenu na kusafirishwa nanyi kwenda Yahudi.

17 Bassi, nilipokusudia haya nalitumia kigeugeu; au niyakusudiayo, nayakusudia kwa jinsi ya mwili illi iwe hivi kwangu, kusema ndiyo, ndiyo, na siyo, siyo?

18 Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu halikuwa ndiyo na siyo.

19 Maana Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, aliyekhubiriwa na sisi kati yenu, na mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa ndiyo na siyo; bali katika yeye ndiyo imepata kuwako.

20 Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo; na katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa kazi yetu.

21 Bassi Yeye atufanyae imara pamoja na ninyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,

22 nae ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.

23 Lakini mimi namwitia Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijaenda Korintho.

24 Si kwamba tunatawala imani yenu; hali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana mnasimama kwa imani.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo