2 Timotheo 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake; 2 likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 3 Maana ntakuja wakati watakapoikataa elimu yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, 4 nao watajiepusha na kusikia yaliyo kweli watageukia hadithi za uwongo. 5 Bali wewe erevuka katika yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mwinjilisti, timiliza khuduma yako. 6 Maana mimi sasa namiminwa, na siku ya kufunguliwa kwangu imekaribia. 7 Nimevifanya vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8 baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake. 9 Jitahidi kuja kwangu upesi; 10 maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu wa sasa, akasafiri kwenda Thessaloniki; Kreske Galatia, Tito Daimatia. 11 Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe; maana anifaa kwa kazi ya khuduma. 12 Lakini Tukiko nalimpeleka Efeso. 13 Joho lile nililomwachia Karpo Troa, ujapo, lete, navyo vitabu, zaidi vile vya ngozi. 14 Iskander mfua shaba alinionya mabaya mengi; Bwana atamlipa kwa jinsi ya matendo yake. 15 Nawe ujibadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu. 16 Katika jawabu yangu ya kwauza hakuna mtu aliyesimama pamoja nami, bali wote waliniacha; wasihesabiwe khatiya kwa jambo bili. 17 Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, illi kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, mataifa wrote wakasikie; nikaokolewa katika kanwa la simba. 18 Na Bwana ataniokoa na killa neno baya na kunihifadhi hatta uje ufalme wake wa milele. 19 Nisalimie Priska, na Akula, na nyumba ya Onesiforo. Erasto alikaa Korintho. 20 Trofimo nalimwacha Mileto, hawezi. 21 Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi. Eubulo akusalimu, na Pudente, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia. 22 Bwana Yesu Kristo awe pamoja na roho yako. Neema na iwe nanyi. Amin. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania